Prof Kitila Mkumbo Atembelea Mtambo wa Ruvu Juu

Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi wa Mamlaka ya Maji Safi na Majitaka (DAWASA), Bw. Romanus Mwangingo (aliyevaa tai) akimpa maelezo Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo (Kushoto) kuhusu maendeleo waliyofanya katika kusambaza maji kwa wananchi wakati wa ziara yake ya kikazi katika eneo la tanki lililopo Kibamba 19 Aprili, 2017.

Continue reading “Prof Kitila Mkumbo Atembelea Mtambo wa Ruvu Juu”

Dk Wilson Ngwale Apewa Uwenyekiti Bodi ya TBA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Waziri wa Ujenzi, Uchukukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mnyaa Mbarawa (Mb), kwa mamlaka aliyopewa kwa mujibu wa Sheria ya Wakala wa Serikali Na. 30 ya mwaka 1997 pamoja na marekebisho yake kupitia Sheria Na. 13 ya mwaka 2009 amemteua Dkt. Edward Wilson Ngwale kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe 10.04.2017.

Mh. Prof. Makame Mnyaa Mbarawa.

Mhe. Prof. Mbarawa amemteua Dkt. Ngwale kushika nafasi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka mitatu katika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi baada ya uteuzi wa awali kufika ukomo.
Aidha, sambamba na uteuzi huo Prof. Mbarawa amewateua Wajumbe watano (5) wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Majengo Tanzania kuanzia tarehe 10.04.2017 kama ifuatavyo:-
1. Eng. John Bura – Mkandarasi kupitia Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB)
2. Arch. Pius P. Tesha – Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
3. Prof. Bakari M. M. Mwinyiwiwa – Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
4. Bw. Ntuli Lutengano Mwakahesya – Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
5. Eng. Amiri N. Mcharo – Wizara ya Fedha na Mipango.

Imetolewa na;

Eng. Joseph M. Nyamhanga
KATIBU MKUU (UJENZI)
12.04.2017

Rais Magufuli Amteuwa Jenerali Venance Mabeyo Mkuu wa Majeshi Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Luteni Jenerali Venance Salvatory Mabeyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Luteni Jenerali Venance Salvatory Mabeyo.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli, leo Tarehe 02 Februari, 2017 amemteua Luteni Jenerali Venance S. Mabeyo kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania. Continue reading “Rais Magufuli Amteuwa Jenerali Venance Mabeyo Mkuu wa Majeshi Tanzania”

Rais Dk. Magufuli Arejea, Apokewa na Makamu Rais

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan va viongozi wengine mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Addis Ababa, Ethiopia, alikohudhuria Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika February 1, 2017.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipungia wananchi mikono alipowasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Addis Ababa, Ethiopia, alikohudhuria Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika February 1, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipungia wananchi mikono alipowasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Addis Ababa, Ethiopia, alikohudhuria Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika February 1, 2017.

Continue reading “Rais Dk. Magufuli Arejea, Apokewa na Makamu Rais”

Global Peace Foundation Tanzania: wazazi jengeni mahusiano mazuri kuleta amani.

Wazazi wa kitanzania wametakiwa kujenga misingi malezi bora ya malezi ili kuleta amani ndani na nje ya familia.

img_1306

Akizungumza mapema leo katika mjadala ambao umefanyika katika zahanati ya Tandale jijini Dar es salaam mkurugenzi mkazi wa Global Peace Foundation Tanzania Martha Nghambi amesema kuwa wazazi ni lazima washiriki kikamilifu katika kujenga misingi ya malezi. Continue reading “Global Peace Foundation Tanzania: wazazi jengeni mahusiano mazuri kuleta amani.”

Mama Janeth Magufuli: Muenzini Mwalimu Nyerere kwa kuwahudumia wazee

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akisalimiana na Viongozi wa Serikali na Chama Mkoani Morogoro alipofika kutembelea makazi ya kulea wazee ya Chazi yaliyopo Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro.

1

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akitembelea na kukagua makazi ya Wazee ya Chazi yaliyopo Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro
Baadhi ya Misaada iliyokabidhiwa kwa wazee wanaoishi katiika makazi ya Chazi yaliyopo Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akisaini kitabu cha wageni alipofika kutembelea makazi ya kulea wazee ya Chazi yaliyopo Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro, Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akicheza mziki pamoja na Viongozi wa Serikali wa Mkoa, Chama na baadhi ya wazee alipofika kutembelea makazi ya kulea wazee ya Chazi yaliyopo Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro.
Baadhi ya Wazee wakimsikiliza Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli alipofika kutembelea makazi ya kulea wazee ya Chazi yaliyopo Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro wakitoa heshima kumuenzi Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Baadhi ya Wazee wakimsikiliza Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli alipofika kutembelea makazi ya kulea wazee ya Chazi yaliyopo Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro.
Kaimu Afisa Mfawidhi wa Makazi ya Kulea Wazee ya Chazi Bw. Rashid Kamwana akisoma risala kwa Mama Janeth Magufuli ambapo aliishukuru serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli kwa kuwajali na kuwahudumia wazee.
Kaimu Afisa Mfawidhi wa Makazi ya Kulea Wazee ya Chazi Bw. Rashid Kamwana akimkabidhi Mama Janeth Magufuli Risala aliyoisoma kuhusu makazi ya kulea wazee ya Chazi yaliyopo Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro yenye jumla ya wazee 28 walioko ndani ya kambi na 162 walioko nje ya kambi.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe akiongea wakati wa ziara ya Mama Janeth Magufuli katika makao ya wazee ya Chazi na kuahidi kuendelea kutekeleza kwa vitendo ahadi ya serikali ya kuwahudumia wazee na watu wasiojiweza katika mkoa wake.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiongea wakati wa ziara yake ya kutembelea makao ya wazee ya Chazi na kuwaasa watanzania kumuenzi Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kuwahudumia na kuwapatia mahitaji muhimu wazee nchini kwa ajili ya ustawi wa maisha yao.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akimkabidhi zawadi ya vyakula muwakilishi wa wazee katika makao ya kulea wazee ya Chazi yaliyopo Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro Bw. Abdalah Mbena
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akipokea misaada mbalimbali kutoka kwa wadau kwa ajili ya wazee wanaoishi katika makao ya wazee ya Chazi yaliyopo Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro.
Muwakilishi wa wafanyakazi katika Makao ya Wazee ya Chazi yaliyopo Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro akimkabidhi zawadi mkungu wa ndizi Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli alipotembelea Makao hayo mapema leo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe akimkabidhi zawadi Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli kwa ajili ya wazee katika makao ya wazee ya Chazi.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akisalimiana na Wazee alipofika kutembelea makazi ya kulea wazee ya Chazi yaliyopo Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe wakiwa katika picha ya pamoja na wazee wanaoishi katika makazi ya kulea wazee ya Chazi yaliyopo Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akisalimiana na watoto alipofanya ziara katika makao ya wazee ya Chazi yaliyopo Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na watoto alipofanya ziara katika makao ya wazee ya Chazi yaliyopo Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro.

PICHA/HABARINA HASSAN SILAYO

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli amewataka watanzania kumuenzi kwa vitendo Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kuwahudumia Wazee nchini kwa kuwapatia mahitaji ya muhimu kwa ajili ya ustawi wa maisha yao.

Akiongea na Wazee katika Kambi ya kulea wazee ya Chazi iliyopo Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro Mama Janeth amesema kuwa watanzania wanapaswa kutambua Wazee ni kundi muhimu kwa ustawi wa nchi kwani miongoni mwao walishiriki katika ukombozi wa taifa leo hivyo tuitumie Siku kama ya leo na nyingine kumuenzi Hayati mwalimu Julius Nyerere akiwa kama mzee aliyetangulia mbele za haki.

“Leo ni siku muhimu sana katika taifa letu siku ambayo tunaenzi siku aliyofariki muasisi awa Taifa letu Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, hivyo ni rai yangu kwa watanzania kwa ujumla kumuenzi kwa kushiriki kwa pamoja katika kuwahudumia wazee na kuwapatia mahitaji yao muhimu” Alisema Mama Janeth.

Aidha, Mama Janeth alisema kuwa amesikia changamoto zinazokabili Makazi hayo na ameahidi kuendelea kushirikiana na wadau kwa kadri iwezekanavyo ili kuhakikisha wanapunguza na kuondoa kabisa changamoto hizo iwe makazi ya wazee Chazi na yote nchini yawe sehemu salama ya kuwahudumia wazee.

Katika kutembelea kituo hicho Mamam Janeth Magufuli ametoa zawadi ya mchele, Maharagwe,unga na mafuta ya kupikia kwa ajili ya wazee na watu wasiojiwezakatika kituo hicho.
Akimkaribisha Mgeni Rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe amesema kuwa serikali ya mkoa wake inatekeleza kwa vitendo maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. john Pombe Magufuli  ya kuwahudumia wazee na kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ndani mkoa wameshaanza kutatua baadhi ya kero na wataendelea kufanya hivyo ili kuyaimarisha makazi ya wazee mkoani humo.

Pia Dkt. Kebwe amewataka watu wote waliovamia makazi ya wazee kuondoka mara moja na kutafuta maeneo mengine na atakayekiuka agizo hilo serikali itamchukulia hatua kali za kisheria.

Akiwasilisha Risala ya Makazi ya Ya wazee ya Chazi kwa Mama Janeth Magufuli Kaimu Afisa Mfawidhi wa Makazi hayo Bw. Richard Kamwana amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa misaada aliyoitoa kwa wazee wa kituo hicho wakati wa sikukuu ya Eid.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Bw. Florent Kiombo amemuhakikishia Mama Janeth Magufuli wataendelea kushirikiana na taasisi nyingine katika kukiendeleza kituo hicho ikiwamo kuwapatia wazee wote kadi za CHF kwa ajili ya kuwasaidia wazee hao kupata huduma ya Afya popote waendapo.

Samia Suluhu: Wananchi wafichueni ambao wanafuja pesa za serikali

MAKAMU wa rais ,Samia Suluhu Hassan,amewataka kuwafichua watumishi mbalimbali wa halmashauri na taasisi za serikali katika wilaya na mikoa wanaodhaniwa kufuja fedha za serikali na kupoteza mapato lengo ikiwa ni kuzikusanya fedha na kuzirudisha katika mikono ya wananchi waone faida yake.
1
Amesema serikali ya awamu ya tano inaendelea na nguvu yake ya kukusanya mapato na kuziba mianya ya rushwa na kupotea kwa mapato.
Aidha Samia ametoa rai kwa wananchi mkoani Pwani kuendelea kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kulinda amani na usalama wa mkoa huo kufuatia  kujitokeza kwa mambo ambayo yameonekana kuhatarisha usalama wa mkoa hivi karibuni.
Katika hatua nyingine amewahakikishia wakazi wa mji wa Chalinze kutatua tatizo la maji ambalo bado ni kero kubwa ambapo ameeleza kwamba mwishoni mwa mwaka huu matunda yataanza kuonekana.
Akizungumza na baadhi ya wananchi wa Mlandizi na Chalinze,mkoani Pwani wakati aliposimama kuwasalimia akielekea mjini Dodoma kikazi,alisema wananchi waiamini serikali yao kwani imeanza kuirejesha nchi katika nidhamu ya mapato na matumizi na kazi ya maendeleo inaendelea.
“Watanzania watajenga Tanzania yao wenyewe na serikali yake na Tanzania inaweza kujiendesha yenyewe na kama itategemea misaada iwe sio kwa kiasi kikubwa.”alisema.
Aliwasisitiza wananchi kulipa kodi pale inapohitajika ili kusaidia na serikali kuinua mapato yake.
Hata hivyo Samia aliwataka wakulima na wafugaji kuishi kwa upendo na mshikamano baina yao pasipo kutofautiana kwani kwa kufanya hivyo kunasababisha migogoro isiyo na tija na wakati mwingine kuvunja amani.
Kufuatia ombi la Mbunge wa jimbo la Chalinze ,Ridhiwani Kikwete ,kumweelezea kuhusu kero ya maji inayowakabili wakazi wa jimbo hilo,Samia alisema serikali inatambua hilo na kwasasa ipo katika mpango mzuri wa kumaliza tatizo la maji lililopo.
Alielezea kuwa WAMI yapo maji ya kutosha lakini tatizo ni usambazaji ,hivyo wanatarajia kuvuta maji kwa mabomba hadi eneo la Pera na kujenga matanki makubwa yenye ujazo wa lita 300,000 ,Kibiki watajenga tanki lenye ujazo wa lita 200,000 ili maji yakifungwa kuweze kuwa  na maji ya kufikisha kwa wananchi kirahisi.
Makamu huyo wa rais alisema watajenga hifadhi nyingine ya maji pale Mazizi yenye lita mil.2 ambayo itawezesha kutumia maji ndani ya wiki mbili bila kukatika ambapo mpango huo upo njia na tayari mkandarasi yupo na wametanguliza sh.bil 43 ili kazi ianze .
Samia wakati anafanya kampeni ili kuomba kuchagulia kuingia madarakani aliahidi kuwatua akinamama ndoo kichwani kwa kutatua tatizo la maji na kusema anashughulikia suala hilo hadi hapo atakapowaondolea wananachi adha ya kutembea umbali mrefu kusaka huduma hiyo muhimu.
“Nayachukua mambo yote na nitaendelea kuyafanyia kazi ,natambua kilio chenu hasa akinamama ambao huamka usiku ama kutembea umbali mrefu kutafuta maji”alisema Samia.
Akizungumzia suala la afya kuhusu vifaa tiba alisema atazungumza na wizara husika kutatua kero ya vifaa tiba,madawa na watumishi katika kituo cha afya Msoga ili kupunguza mzigo kwa hospitali za rufaa ikiwemo Tumbi.
Alisema tatizo la watumishi karibu litamalizika,kulikuwa na idadi kubwa ya watumishi hewa hivyo walikuwa wakiisafisha watumishi hao na hivi karibuni watafungua ajira mpya baada ya zoezi hilo kukamilika.
Samia aliipongeza Chalinze kumaliza tatizo la madawati ila kwenye mafanikio kunajitokeza tatizo jingine hasa kutokana na idadi ya wanafunzi imekuwa kubwa na kuzalisha tatizo la madarasa .
Aliwataka viongozi wa wilaya na mkoa kuelekeza nguvu zao kujenga ,kuongeza na kukarabati majengo ya madarasa  ili watoto waweze kusoma .
Kuhusiana na ahadi ya ujenzi wa soko na stend mjini Chalinze,amemuagiza mkuu wa mkoa huo,mhandisi Evarist Ndikilo kuhakikisha anasimamia hatua ya tathmini ya eneo lililopatikana kwa ajili ya ujenzi huohadi ifikapo mwezi novemba mwaka huu.
Viwanda na uwekezaji,anasema serikali kwasasa inasuka nguvu za viwanda na uwekezaji mkoani hapo kujenga kwa ajili ya kutengeneza ajira na kukuza uchumi wa mkoa .
Alisema viwanda vikubwa 10 vitajengwa ikiwemo cha chuma na nondo,cha kutengeneza vigae na kusindika matunda  hivyo wananchi wawe tayari kupokea wawekezaji ili kupunguza tatizo la uhaba wa ajira.
Akiwa Mlandizi ,Samia aliahidi kuweka uzio kama alivyoahidi wakati wa kampeni kwenye uchaguzi uliopita katika kituo cha afya Mlandizi  kwani ni moja ya sifa ya kuandishwa kwa kituo cha afya kupanda hadhi ya wilaya na bado wanania ya kupandisha hadhi ya kvituo mbalimbali ili kuzipunguzia mzigo hospitali za rufaa .
Alisema soko la mlandizi bado ni dogo ila ana taarifa kuwa kwenye eneo la Kisabi A na B kuna maeneo yamepimwa kwa ajili ya masoko na Tamisemi wameweka mkono kidogo na kuwahakikishia kuwa atakaa na Tamisemi kuangalia uwezekeno wa kuachia maeneo hayo ili kuwepo na soko na stend kubwa .
Alieleza kupimwa kwa mji wa Mlandizi na kusema  ataongea na wizara ya ardhi na sasa bahati nzuri  wizara hiyo  wamekuwa wepesi kufanya zoezi hilo hivyo ataweka msukumo kwa wizara ili waweze kupimiwa na  barabara ya Mlandizi-Mzenga ahadi ipo palepale itajengwa kwa kiwango cha lami .