Nafumaniwa kila siku – Peter Msechu

Msanii Peter Msechu ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake ‘Yakawa’ amefunguka na kusema mwili wake si tatizo kwani kila siku amekuwa akifumaniwa mtaani na watu akiwa na totozi za watu.

Msechu alisema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha 5 Selekt ambapo alidai licha ya kuwa na mwili mkubwa lakini mwili huo haumsumbui wala kumpa tatizo lolote kama baadhi ya watu wengine wanavyodhani na kusema amekuwa akiupigisha sana mazoezi ndiyo maana yuko fiti.

“Wakati Timbulo anasema mshumaa mambo ya kuachwa mimi na Yakawa yaani na wanawake wengi, mimi nafumaniwa kila siku kwa hiyo mimi na nguvu ya kujitahidi kwenda na mwili wangu huu, mimi nafanya sana mazoezi watu wengine ooh Msechu sijui mnene, mimi wanawake mtaani wanaongozana nasingiziwa kila kukicha watoto eti watoto wangu, kwa hiyo msinichukulie poa niko vizuri kila idara” alisema Msechu

Mbali na hilo Msechu anasema wimbo wake mpya na video yake imempa madeni makubwa kwani pesa zote amekwenda kufanyia video hiyo na kuwataka watu wasiishie tu kutumiana wimbo huo kwenye mitandao bali waangalie kwenye account zake ‘You Tube’ na kununua wimbo huo kwenye mitandao ya kijamii ambako ameuweka ila kumsaidia kupata fedha za kulipa madeni hayo.

Itazame hapa ngoma mpya ya Peter Msechu

Timbulo awataka wasanii wasimlilie

Mwanamuziki anayetamba na ngoma ya ‘Mshumaa’, Timbulo amewataka wasanii wasipate presha kipindi hiki ambacho yeye anaachia ngoma mara kwa mara kwani alikaa nje ya ‘game’ muda mrefu hivyo sasa anafanya kazi kwa bidii ili kwenda sawa na waliopo sokoni.

Akizungumza kwenye 5Selekt ya EATV , Timbulo amesema kwamba yeye ni mfuasi wa muda hivyo kipindi alichokuwa amekaa kimya wasanii wengine walikuja na kufanya vizuri hivyo sasa ni muda wake kuwaonyesha uwezo wake lakini wameanza kuogopa na kulalamika.

“Sasa hivi nimeamua kutoa vyuma ili niende sawa na wenzangu waliokuwepo kwenye game, kuna baadhi ya wasanii mpaka wanalia wananiambia mbona sasa unazidisha kila siku wewe tu unaachia ngoma mpya, nawaambia tulieni nataka tuende sawa maana wao wameshaniacha mbali sitakiwi tena kutembea.

Kwa upande mwingine Timbulo amesema kwamba hafahamu ukubwa alionao Tanzania kwani bado anajiona hajafika mahali ndio maana anakaza kupambana kila siku

“Mimi sijui ukubwa wa jina langu, watu wa nje huko ndio wanafahamu nina ukubwa gani. Watu wanapohoji umri niliokuwepo kwenye game na ukubwa wa jina langu mimi nitawajibu na deserve kuwa hivi kwani mimi nilikaa kimya muda mrefu nikawaacha wengine wafanye, lakini namshukuru Mungu bado watanzania wananipa sapoti ya kutosha”. Aliongeza.

Pamoja na hayo Timbulo amesema anaamini huu ndio muda wake sahihi wa kung’aa ingawa alikuwa kimya muda mrefu kwenye ‘game’.

“Mimi ni muasisi mzuri wa muda, kung’aa kwangu siyo kwamba nimebadilisha uongozi, waliokuwa wakinisimamia toka naanza muziki ndio mpaka saivi nipo nao ingawa wapo wasanii kibao walioondoka na kutukana kwamba management haina pesa. Hivyo sasa hivi kuonekana nafanya poa ni kwa sababu muda wangu umefika wa kung’aa”, T imbulo alisema

Continue reading “Timbulo awataka wasanii wasimlilie”

HIVI Ndivyo Nay wa Mitego Alivyonusurika Kutekwa na Watu Wasiojulikana Dar..!!

nay-wa-mitego-pale-kati-patamuWAKATI hofu ya kutekwa ikiwa juu, msanii wa Hip Hop Bongo, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amenusurika kutekwa na watu wasiojulikana, Risasi Jumamosi lina habari kamili. Kwa mujibu wa chanzo makini, Nay alipatwa na maswaibu hayo mwishoni mwa wiki iliyopita wakati alipokuwa anatoka kwenye shoo aliyoifanyia Kigamboni jijini Dar.

Continue reading “HIVI Ndivyo Nay wa Mitego Alivyonusurika Kutekwa na Watu Wasiojulikana Dar..!!”

RC MAKONDA ; NIMARUFUKU KUUZA CD BILA KIBALI,AU KITAMBULISHO KATIKA MKOA WA DSM, ATAJA MAJINA 13 YA VINARA NA KUAMURU WARIPOTI POLISI CENTRAL IJUMAA

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam  Mhe.Paul Makonda amewataka wote wanaofanya biasha ya kuuza CD na DVD kwa kutembeza mtaani  mkononi pamoja na wanaodurufu kazi za   wasanii kuacha  maramoja kabla hawaja chukuliwa hatua za kisheria .

16-1

Akizungumza katika maandamano ambayo yaliratibiwa na wasanii wa filamu na na kuhusisha ofisi ya mkuu wa mkoa na Wizara ya Habari utamadun sanaa na Michezo Continue reading “RC MAKONDA ; NIMARUFUKU KUUZA CD BILA KIBALI,AU KITAMBULISHO KATIKA MKOA WA DSM, ATAJA MAJINA 13 YA VINARA NA KUAMURU WARIPOTI POLISI CENTRAL IJUMAA”

MTANZANIA APATA NAFASI YA JUU YA KUONGOZA MULTICHOICE TANZANIA

Kama mojawapo ya makampuni ya Afrika yanayoongoza katika sekta ya burudani za video, MultiChoice inatambua kwamba rasilimali watu ni kitovu cha simulizi ya mafanikio yake-ndio maana inawekeza sana katika kutafuta, kuendeleza na kunoa watu bora kabisa katika sekta. Kama kampuni ya kimataifa, falsafa yetu ya kufikiri kimataifa na kutenda kwa ndani ya nchi inaungwa mkono na programu za kuendeleza utendaji wenye nguvu na sera ambazo zimejizatiti katika kuendeleza biashara za ndani na kuajiri watu kutoka miongoni mwa vipaji vilivyolelewa na kukulia nchini.

index

MultiChoice Tanzania inayo furaha kutangaza uteuzi wa Bw. Maharage Ally Chande kama Mkurugenzi Mtendaji mpya wa MultiChoice Tanzania. Chande anajiunga na familia ya MultiChoice baada ya hapo awali kushika wadhifa wa Mkurugenzi Wa Huduma Za Taasisi katika Ofisi Ya Rais-Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Miradi ( President’s Delivery Bureau). Continue reading “MTANZANIA APATA NAFASI YA JUU YA KUONGOZA MULTICHOICE TANZANIA”

Harmonize asema Jackline Wolper alikuwa Single

Wcb staa Harmonize amesema alimkuta mpenzi wake Jackline Wolper akiwa single, ndiyo maana wakaweza kuanzisha mahusiano.

Harmonize amesema hayo kupitia kipindi cha Enews ambapo alikuwa anaelezea mambo mbalimbali kuhusu maisha yake mapya katika mahusiano na Wolper ambaye yeye mwenyewe amekiri kuwa ni mtu aliyeanzisha naye mahusiano hivi karibuni na kusema tuwe na subira kila kitu kitakuja kuwekwa wazi siku za usoni. Continue reading “Harmonize asema Jackline Wolper alikuwa Single”