Wapenzi wa jinsi moja kukosa huduma Mississippi

Nchini Marekani, gavana wa jimbo la Mississippi amepitisha sheria kuwaruhusu wafanya biashara kutowauzia bidhaa zao wapenzi wa jinsi moja endapo imani zao hazikubaliani na suala hilo.

 130919124115_gay_activist_ukraine_512x288_afp

Gavana huyo kutoka katika chama cha Republican Phil Bryant ametia saini sheria hiyo pamoja na kukabiliana na upinzani mkali kutoka katika jamii hiyo ya wapenzi wa jinsi moja pamoja na mashirika mbalimbali ambao wanaona kwamba sheria hiyo ni ya kibaguzi. Continue reading “Wapenzi wa jinsi moja kukosa huduma Mississippi”

Gardner ashindwa kitendawili cha ‘NDI NDI NDI’

Ilikuwa ni mwendo wa majibu ya mkato na mafumbo kutoka kwa Gadner tulipotaka atupe mtazamo wake juu ya hit song “NDI NDI NDI” ya Jay Dee.

Camera ya ENewz ilikutana na aliyekuwa mume na pia meneja wa mwanadada Lady Jay Dee, Gadner G Habash na kutaka kupata mtazamo wake juu ya wimbo mpya wa Lady Jay Dee wuitwao “Ndi Ndi Ndi”, hii ni kutokana stori kuzagaa mitaani kuwa “Ndi Ndi Ndi” ilikuwa ni fumbo kwa Gadner.

Gadner alikataa kuzungumzia chochote kuhusu nyimbo hiyo na kusema “Si ajabu watu wakinishangaa kwa hili, kama kushangaa watu wanashangaa hata mlima Kilimanjaro ambao upo kila siku.

Continue reading “Gardner ashindwa kitendawili cha ‘NDI NDI NDI’”

The power of Women .. Hilda Ngaja Talk kujiwekea mazoea ya kujipangia ratiba ya kia siku ili kutimiza malengo yako

watu wengi wamekuwa wakifeli kufikia malengo yao kwa kuwa wamekosa mazoezi ya kujiwekea mazoea ya kujipangia ratiba za kila siku za mipango katika maisha yao.

kwa mara nyingine tena mkurugenzi na mwanzilishi wa kampuni ya Hidelly solutions Hilda Ngaja leo anatoa soma la namna ya kujiwekea mazoea ya kujipangia ratiba ya kia siku ili kutimiza malengo yako.

Kupanda na kushuka kwa simu za Nokia

Je, unaikumbuka siku za Nokia na enzi zake? Sasa Jina Nokia linatokaka na mji mdogo nchini Finland, ambapo simu hiyo iliyokuwa maarufu duniani iligunduliwa.

 160318142506_nokiagofigure3

Kuna dalili kidogo kuwa mji huo mtulivu wakati mmoja uliipa simu jina lake, simu ambayo ilibadili kabisa sekta ya simu mapema miaka ya tisini na kubadilisha kabisa uchumi wa Finland kuufanya kuwa uchumi ulioboreka kwa haraka zaidi duniani. Continue reading “Kupanda na kushuka kwa simu za Nokia”

Nike yazindua viatu vinavyojifunga kamba

Kampuni ya Nike imezindua viatu vinavyojifunga kamba zake vyenyewe.Inadaiwa kuwa viatu hivyo vitatolewa kwa uma kabla ya mwisho ya mwaka huu.

 160318112738_nike_512x288_bbc_nocredit

Viatu vinavyojifunga kamba zake vyenyewe vilionekana katika filamu ya Future II mwaka 1989,lakini ndoto ya utengenezaji wa viatu hivyo ikaanza kuafikiwa mwaka 2013 ambapo Nike ilianza kuvitengeza viatu hivyo.

Continue reading “Nike yazindua viatu vinavyojifunga kamba”

Picha ya utupu wa Kim Kardashian yafutwa Australia

Picha iliochorwa ya utupu wa Kim Kardashian imefutwa siku chache tu baada kuchorwa na msanii mmoja mjini Melbourne nchini Australia.

 

Picha hiyo ilichorwa na msanii Lush Sux katika ukuta mmoja wa makaazi ya mji huo.

Lakini picha hiyo yenye urefu wa mita 10 ilirushiwa rangi mbali na kuwekewa maandishi machafu yalioandikwa chini yake.

Lush Sux ambaye jina lake ni Mark Walls aliwaambia wapita njia kwamba alikasirishwa kuona kuwa mchoro huo umemwagiwa rangi.

”Niliona umuhimu wa kuichora picha hii mara moja nilipoiona katika mtandao wake wa Instagram hadharani,katika jengo moja la ghorofa tatu”.

”Pengine pia mimi hupenda kuangaziwa kama yeye”.Picha hiyo ilichorwa katika ubavu wa ukuta mmoja unaomilikiwa na kampuni ya uchoraji ya Melbourne.

Ukuta mwegine uliopo mkabala na picha iliomwagiwa rangi una picha ya mgombea wa urais wa Marekani Donald Trump.

Kim Kardashian alikosolewa kwa kuweka picha hiyo ya utupu katika mtandao wa instagram katika siku ya kimataifa ya wanawake .

Aliwashtumu wakosoaji wake akisema imetosha kwa kuuaibisha mwili wake.

Aliwaambia mashabiki katika mtandao wake :”Mimi ni mama,mimi ni mke wa mtu,mimi ni dada na mtoto wa mtu,mfanyibiashara na ni haki yangu kuwa na umbo la kuvutia.Mwili wangu umenipa fursa hiyo,na jinsia yangu.Nimepewa fursa ya kuuonyesha ulimwengu kuhusu nilivyo na siogopi kile mtu yeyote atakachosema.Nachukua fursa hii kuwashinikiza wasichana na wanawake duniani kufuata nyayo zangu”