Q Chief ajiweka pembeni na uongozi wa Bendi

Msanii Q Chief ambaye sasa yupo chini ya Bendi mpya ya Q S Mhonda, ameeleza kuwa licha ya uzoefu wake katika muziki kwa miaka, amejiweka pembeni na jukumu la kuongoza bendi hiyo mpya kutokana na lawama nyingi ambazo huambatana na nafasi hiyo.

Q chief amesema kuwa, anasaidia bendi yake hiyo kwa kuwakutanisha na wasanii na wadau mbalimbali kuwapa semina wasanii ambao atakuwa akifanya nao kazi katika bendi hiyo ambayo itazinduliwa rasmi kwa tukio kubwa la onyesho la burudani jumapili hii.

Akizungumzia uzoefu wake, Q Chief amesema kuwa kuishi na wanamuziki kunahitaji moyo, akiwa sasa amekwishaweka mambo yake sawa tayari kwa kuendesha shughuli zake na bendo hiyo, jukumu ambalo atalifanya sambamba na safari yake kama “Solo Artist’.

Continue reading “Q Chief ajiweka pembeni na uongozi wa Bendi”

New Music: Rick Ross – ‘AMAZING GRACE’

Baada ya kuachia video yake mpya ya wimbo wa Sorry siku mbili zilizopita Rick Ross ameachia Track nyingine mpya called “Amazing Grace,” ambayo ni moja kati ya Tracks zilizopo kwenye album yake mpya ‘Black Market’ ambayo bado haijatoka hivyo basi ukiwa kama shabiki wa ukweli na mdau wa muziki hapa ndio pake Tumia dakika zako kadhaa kuisikiliza hii track hapa ukimaliza tunakuomba usibanduke kwenye tovuti yetu kwanin bado tunaendelea kukuuza zaidi. Mtaarifu na mwenzio

Alikiba na Christian bella wasema anayetaka kufanya filamu ya ‘Nagharamia’ awe na Million 700, wimbo wao kutoka Ijumaa hii

Ijumaa ya wiki hii Alikiba na Christian bella watakata kiu ya mashabiki wao kwa kuachia collabo yao inayosubuliwa kwa hamu zaidi.

Kwa upande mwingine, Alikiba na Christian bella wamesema story ya wimbo wao inavutia kiasi kwamba unaweza tengenezea filamu lakini.

Bella na Ali Kiba

“Nyimbo tuliyoimba inaweza ikawa hata sound track ya movie kwasababu ni story ambayo inavutia, inapendeza…” Alikiba alifunguka kupitia 255 ya XXL. “Ni idea nzuri ambayo inahitaji hata kufanyiwa movie ikipata nafasi vile vile uwezekano huo wa kufanya upo.

Kiba na Bella wametoa nafasi kwa mtu ambaye atapenda kutengeneza filamu kupitia idea ya wimbo wao lakini awe na Million 700 mezani kwasababu washasajili wazo lao.

“Akija na mtonyo akiweka mtonyo tutafanya tu” alisema Bella. “Kwa haraka haraka labda milioni 700 hivi” aliongezea Kiba.

Ichi ni kionjo cha wimbo huo.