Abiria wa Bombadier Mwanza- Bukoba wakwama -VIDEO

Dar es Salaam. Ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) iliyoondoka saa 12:00 asubuhi Dar es Salaam kwenda Bukoba kupitia Mwanza, imekwama jijini Mwanza baada ya kupata hitilafu. Kuharibika kwa ndege hiyo kumesababisha abiria waliokuwa wakielekea Bukoba kukwama hadi sasa bila kuelezwa hatima yao.   Akizungumza kwa simu, mmoja wa abiria ambaye alikuwa anaelekea kwenye msiba wa shemeji yake kutokea Mwanza, Muhiddin Khalid alisema … Continue reading Abiria wa Bombadier Mwanza- Bukoba wakwama -VIDEO

Diamond Platunumz afunguka mazito kuhusu mtoto wa Hamisa Mabeto

Dar es Salaam. Mwanamuziki Diamond Platnumz amesema uhusiano wake na mwanamitindo Hamisa Mobeto umeidhalilisha familia yake hasa mama yake na mzazi mwenzake Zarina Hassan, maarufu Zari. Akizungumza katika kipindi cha Leo Tena kinachorushwa na kituo cha Redio cha Clouds jijini Dar es Salaam leo Jumanne, Diamond amesema mama yake alitukanwa katika mitandao ya kijamii baada ya kumtembelea mwanamitindo huyo alipojifungua takribani wiki sita zilizopita.   … Continue reading Diamond Platunumz afunguka mazito kuhusu mtoto wa Hamisa Mabeto

Diamond: Nilitaka mwanangu aitwe Dylan nashangaa kuitwa Abdul

Dar es Salaam. Mwanamuziki Diamond Platnumz amesema jina alilotoa apewe mtoto wake kwa Hamisa Mobetto ni Dylan lakini kwa sababu za kutafuta umaarufu mwanamke huyo alimwita Abdul Nassib.   Amesema Hamisa alimwita mtoto huyo Abdul ambalo ni jina la baba yake mzazi ili iwe rahisi watu kufahamu kuwa mtoto huyo ni wa kwake baada ya kukubaliana kufanya uhusiano wao kuwa wa siri.   “Mimi jina … Continue reading Diamond: Nilitaka mwanangu aitwe Dylan nashangaa kuitwa Abdul

Neema Mwasyeba: Mwanamke unatakiwa kuwa chanya

Wanawake wa kitanzania wameaswaa kuacha tabia ya kulalamika na kuchangamkia fursa zilizopo ili kwendana na kasi ya maisha ya ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia. Hayo yamezungumzwa katika uzinduzi wa programu ya Mwanamke Chanya “Mentorship Programu” iliyofanyika Leo Jijini Dar es salaam, Programu hiyo yenye lengo la kumuinua na kumpa nguvu mwanamke katika ujasiriamali, uhusiano. Programu hiyo ambayo imeandaliwana Neema imezinduliwa leo itakuwa ikifanyika kwa … Continue reading Neema Mwasyeba: Mwanamke unatakiwa kuwa chanya

IGP SIRRO AWATAHADHARISHA WANAOTOA TAARIFA ZA UONGO JUU YA SHAMBULIO LA LISSU

Jeshi la Polisi Nchini limewata wananchi kuacha kusambaza ujumbe,picha au video na taarifa zisizo na ukweli kwenye mitandao  kuhusiana na tukio la kushumbuliwa kwa risasi Tundu Lissu. Hayo yamesemwa  na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro wakati wa mkutano wake na wanahabari jijini Dar es salaam. IGP Sirro amesema kuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria huku akiwsomba wananchi kuendelea kutoka ushirikiano kwa jeshi … Continue reading IGP SIRRO AWATAHADHARISHA WANAOTOA TAARIFA ZA UONGO JUU YA SHAMBULIO LA LISSU

Hizi ndio sababu za Lissu kutibiwa Nairobi

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai, ametolea ufafanuzi suala la matibabu ya mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Mh. Tundu Antiphas Lissu aliyepelekwa Nairobi nchini Kenya baada ya kupigwa risasi. Akitoa taarifa hiyo mara baada ya sala ya kuliombea bunge asubuhi ya leo ili kuanza vikao, Spika Ndugai amesema utaratibu wa matibabu kwa mbunge yeyote ulikuwa … Continue reading Hizi ndio sababu za Lissu kutibiwa Nairobi

Alichokisema Nape Baada ya Tukio la Lissu

Aliyekua Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amefunguka na kumuombea Mbunge Tundu Lissu ili aweze kupona na kuja kueleza ukweli juu ya watu ambao wamemfanyia kitendo hicho cha kinyama. Mbunge wa Mtama Nape Nnauye na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu walipokutana jana kabla ya mbunge huyo kupigwa risasi na watu wasiojulikana. Nape Nnauye jana kabla … Continue reading Alichokisema Nape Baada ya Tukio la Lissu

Maaskofu kurudisha mgao wa Escrow

Askofu Msaidizi jimbo la Bukoba, Mhashamu Method Kilaini pamoja na Mhashamu Eusebius Nzigilwa wa jimbo kuu katoliki la Dar es salaam wamefunguka na kutoa taarifa kuwa wameamua kurudisha mgao wa fedha za Escrow ambazo walipewa na James Rugemalira. Viongozi hao wa dini wamesema wameamua kurudisha fedha hizo za serikali kutokana na kuwepo kwa kesi mahakamani ya kuhujumu uchumi inayomkabili James Rugemalira ambaye ndiye aliwapa fedha … Continue reading Maaskofu kurudisha mgao wa Escrow

Abby Dady afunguka kuvujisha wimbo wa Alikiba

Producer wa muziki wa bongo fleva Abby Dady amesema kitendo cha kuvujisha wimbo wa Alikiba ambao amekuwa akituhumiwa kwamba ameuvujisha, amesema hawezi kufanya hivyo kwani kitamuharibia kibiashara Akizungumza kwenye eNewz ya East Africa Television, Abby Dady amesema yeye kama producer na mfanya biashara lazima alinde kazi zake na kutengeneza wasifu mzuri, kwani bila hivyo itakuwa inamuharibia kwenye soko la kazi zake. “Hicho kitu kitaniharibia biashara watu … Continue reading Abby Dady afunguka kuvujisha wimbo wa Alikiba

Rais Magufuli atoa tamko tukio la Lissu

Rais John Magufuli amesikitishwa na taarifa alizozipata tukio la kupigwa kwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu akiwa nyumbani kwake Dodoma leo na kuviagiza vyombo vya dola viwasake waliyofanya uhalifu huo. Rais Magufuli amesema hayo kupitia ukurasa wake wa twitter jioni ya leo na kutaka vyombo vya usalama kuwatafuta watu waliofanya tukio hilo la kinyama. “Nimepokea kwa masikitiko tukio la kupigwa risasi Mh.Tundu … Continue reading Rais Magufuli atoa tamko tukio la Lissu