HIVI Ndivyo Nay wa Mitego Alivyonusurika Kutekwa na Watu Wasiojulikana Dar..!!

nay-wa-mitego-pale-kati-patamuWAKATI hofu ya kutekwa ikiwa juu, msanii wa Hip Hop Bongo, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amenusurika kutekwa na watu wasiojulikana, Risasi Jumamosi lina habari kamili. Kwa mujibu wa chanzo makini, Nay alipatwa na maswaibu hayo mwishoni mwa wiki iliyopita wakati alipokuwa anatoka kwenye shoo aliyoifanyia Kigamboni jijini Dar.

Continue reading “HIVI Ndivyo Nay wa Mitego Alivyonusurika Kutekwa na Watu Wasiojulikana Dar..!!”

Gardner ashindwa kitendawili cha ‘NDI NDI NDI’

Ilikuwa ni mwendo wa majibu ya mkato na mafumbo kutoka kwa Gadner tulipotaka atupe mtazamo wake juu ya hit song “NDI NDI NDI” ya Jay Dee.

Camera ya ENewz ilikutana na aliyekuwa mume na pia meneja wa mwanadada Lady Jay Dee, Gadner G Habash na kutaka kupata mtazamo wake juu ya wimbo mpya wa Lady Jay Dee wuitwao “Ndi Ndi Ndi”, hii ni kutokana stori kuzagaa mitaani kuwa “Ndi Ndi Ndi” ilikuwa ni fumbo kwa Gadner.

Gadner alikataa kuzungumzia chochote kuhusu nyimbo hiyo na kusema “Si ajabu watu wakinishangaa kwa hili, kama kushangaa watu wanashangaa hata mlima Kilimanjaro ambao upo kila siku.

Continue reading “Gardner ashindwa kitendawili cha ‘NDI NDI NDI’”

Amanda Atumika kwa Utapeli

Staa wa Bongo Movies, Tamrina Posh ‘Amanda’ amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya jina lake kutumika kwa utapeli kwenye mitandao ya kijamii.

Amanda Poshi

Amanda ameliambia Ijumaa Wikienda kwamba, kuna Amanda feki anayetumia jina lake kutapeli watu ambapo tayari amepokea malalamiko mengi huku jamaa mmoja akichukuliwa fedha kilaini (hakutaja kiasi) kupitia Facebook, akiamini ni staa huyo hivyo kuwataka watu kuwa makini kwani yeye hana mchezo huo.

Chanzo: GPL

Video: Meek amtisha Drake kwa video hii tena.

Rapa kutoka Philadelphia Meek Mill amesikika kwenye wimbo wake uliopo kwenye mixtape ya “Dreamchasers 4” akimtishia msanii mwingine aliyetajwa kuwa ni Drake.

meek-drake

Kwenye wimbo huu anamuongelea msanii asiyeandika mashairi yake mwenyewe.

“When I was saying shit about the rhymes you ain’t wrote /  I can’t wait ’til we run in ya / I’ma put a gun in ya,” the Philadelphia emcee raps in the clip.

Meek Mill alimtuhumu Drake kuwa anatumia ghostwriter [waandishi wa wasiotajwa] na Drake alimjibu kupitia nyimbo mbili ambazo zilikuwa “Charged Up” na “Back to Back” na Meek Mill alijibu kwa wimbo mmoja “Wanna Know.”

Meek Mill amekuwa akirekodi mixtape yake ya Dreamchasers 4.

Shamsa Achekelea Mpenzi Mpya

STAA wa filamu Bongo, Shamsa Ford ameonesha furaha yake ya kuumaliza mwaka kwa kumpata mpenzi mpya, ambaye hata hivyo, alikataa kutaja jina lake.

Shamsa Ford

Akizungumza na gazeti hili juzikati, Shamsa alisema mwaka huu pia umeweka historia kwa yeye kuweza kutimiza mambo yote aliyojipangia tangu alipoachana na baba wa mtoto wake.
“Nafurahi sana namaliza mwaka nikiwa nimetimiza malengo pia kuwa na mpenzi mpya ambaye ni mume wangu mtarajiwa, ndani ya mwaka huu nimejifunza siyo vizuri kuweka uhusiano wazi hasa kwenye mitandao ya kijamii, maana unajidhalilisha unaweza kujikuta leo uko na huyu kesho na huyu inakuwa ni aibu,” alisema Shamsa.

Chanzo:GPL

Kendrick Lamar na ScHoolboy Q wakanusha taarifa za kupigana studio.

Rapa Kendrick Lamar na ScHoolboy Q wamekanusha taarifa kuwa walipigana studio weekend hii. Wasanii hawa wa kundi la TDE walitumia twitter kusema kuwa taarifa zilizosamba sio za kweli.

Shabiki aliuliza hivi twitter >>“Aye @dangerookipawaa my cousin was in the studio the other night tellin me Schoolboy q & K Dot got into a scuffle,” he wrote.

Jibu lilikuwa>> “Just having a minor disagreement. Nothing serious.” Ila inasemekana ni kweli walishikana mashati sababu ikitajwa kuwa wakati wa session yao studio Kendrick Lamar alijidai mjuaji sana kutokana na mafanikio yake kitu ambacho School Boy Q hakupenda.

Masika Kalysha asema anaujauzito wa Fetty Wap,ataja hata nyimbo waliosikiliza wakiwa wana DO.

Rapa Fetty Wap aliyetamba duniani kupitia wimbo wake wa Trap Queen tayari ni baba wa watoto wawili Zaviera [Wakike] na Zoovier [Wakiume] na sasa anategemea kupata mtoto wa tatu.

masika-fetty

Kwa mujibu wa kipindi cha “Love & Hip-Hop: Hollywood, mwigizaji wa show hio Masika Kalysha anaujauzito wa Fetty Wap.

Masika aliongea na kipidni cha Power 106 “The Cruz Show” nakusema anaujauzito wa miezi sita na walitengeneza mtoto huyo wakisikiliza wimbo wa Fetty Wap ‘Andale’ kitandani pamoja.

Fetty ametumia twitter yake kukanusha kuwa yeye ni baba wa mtoto huyo na kusema Masika anatafuta umaarufu kupitia yeye. “B*****s posting pics now the world going crazy , she need a come up I understand that career looking bad.”

Wema Sepetu na Diamond kunani ? Wema aweka video akiimba wimbo mpya wa Diamond ‘Utanipenda?’

Mpenzi wa zamani wa Diamond Platnumz, Wema sepetu ni shabiki mkubwa wa wimbo mpya wa msanii huyo ‘Utanipenda’

Screenshot_2015-12-15-05-31-28

Kwenye kipande kifupi cha video kilichowekwa kwenye snapchat ya rafiki kipenzi cha Wema sepetu, Aunty Ezekiel kimeowaoneshwa kwa pamoja wakiimba nyimbo hiyo ambayo imetoka siku tatu zilizopita, Wema na yeye kwenye Snapchat yake aliweka video ya bila sauti huku akiipa Caption ya ‘Je utanipendaga?’ ambayo ni jina la wimbo huo.

Siku chache zilizopita Wema sepetu alionekana akiwa karibu tena na ndugu wa mpenzi wake huyo wa zamani ambaye wana tabia ya kurudiana na kuachana, Romy Jones.

Credits: teamtz