Diego Simeone aongeza mkataba wa hadi mwaka 2020 Atlentico Madrid

Kocha wa Klabu ya Atletico Madrid Diego Simeone amezima tetesi za kuhamia klabu ya Inter Milan ya Italia baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka mitatu kuendelea kufundisha miamba hiyo ya jiji la Madrid. Murgentina huyo alikuwa akihusishwa na kuhamia kwa vigogo hao wa Italia, ambao aliwachezea kuanzia mwaka 1997 hadi 1999, lakini ameamua kujifunga na waajiri wake wa sasa. Simeone anapendwa sana na mashabiki … Continue reading Diego Simeone aongeza mkataba wa hadi mwaka 2020 Atlentico Madrid

SIMBA Wamsafishia Njia Okwi ya Kucheza Ligi Kuu Msimu Ujao..!!!

emmanuel okwi
MSHAMBULIAJI raia wa Uganda, Emmanuel Okwi, sasa amesafishiwa njia ya kutua kwenye klabu yake ya zamani ya Simba ya jijini Dar es Salaam, baada ya uongozi wa timu hiyo kueleza mipango ya kuachana na beki wake raia wa Uganda, Jjuuko Murshid, ili kutoa nafasi kwa mshambuliaji huyo.

Continue reading “SIMBA Wamsafishia Njia Okwi ya Kucheza Ligi Kuu Msimu Ujao..!!!”

Show ya El Classico yamalizwa na Messi sekunde za mwisho.

3F8A376A00000578-0-image-m-24_1492980230901
Mshambuliaji wa  Barcelona na timu ya Taifa ya Argentina Lionel Messi ndio ameonekana kuwa hatari zaidi kwa kumsababishia Sergio Ramos kupata kadi nyekundu ya 22 katika historia yake ya soka kutoka na kumchezea Lionel Messi faulo dakika ya 77, Lionel Messi ndio alikuwa hatari na kufanikiwa kufunga magoli mawili dakika ya 33 na 90 baada ya Ivan Rakitic kufunga goli la pili dakika ya 73.

Continue reading “Show ya El Classico yamalizwa na Messi sekunde za mwisho.”

SIMBA YAIJIA JUU KAMATI YA TFF JUU YA SAKATA LA KAGERA SUGAR, YALIA USIKU NA MCHANA KUTAKA POINT

Wakati kamati ya Sheria,Katiba na Hadhi za Wachezaji ikitaraji kutoa maamuzi muda wowote kuanzia sasa juu ya hatma ya pointi tatu na mabao matatu waliyopewa klabu ya Simba,baada ya klabu ya Kagera Sugar kuwasilisha malalamiko TFF wakipinga maamuzi ya kupokwa pointi tatu na kamati ya saa 72 leo hii uongozi wa Simba umeweka bayana juu ya swala hilo.
IMG_20170419_1213431.jpg
Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii katika makao makuu ya klabu,Mkuu wa idara ya Habari na mawasiliano wa klabu ya Simba,Haji Manara amesema kwamba hakukuwa na haja ya kamati ya Katiba,Sheria na Hadhi za Wachezaji kuitisha kikao kwa ajili ya kujadili marejeo ya shauri la Kagera Sugar kwa madai kuwa haina uhalali wa kufanya jambo hilo.

Continue reading “SIMBA YAIJIA JUU KAMATI YA TFF JUU YA SAKATA LA KAGERA SUGAR, YALIA USIKU NA MCHANA KUTAKA POINT”

KAMATI YA SAA 72 YAIPA SIMBA POINTI TATU KWA UZEMBE WA KAGERA SUGAR

Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi Tanzania, maarufu kama Kamati ya Saa 72 imeipa Simba SC pointi tatu na mabao matatu kutokana na rufaa waliyoikatia Kagera Sugar kwa kumtumia beki Mohammed Fakhi akiwa ana kadi tatu za njano katika mechi baina ya timu hizo Aprili 2, mwaka huu.
IMG-20170413-WA0104-640x427.jpg
Katika mchezo huo ambao Kagera Sugar walishinda mabao 2-1 Uwanja wa Kaitaba, wanadaiwa kukiuka kanuni kwa kumchezesha Fakhi, beki wa zamani wa Simba badala ya mchezaji huyo kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano alizopata mfululizo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Ahmed Yahya amewaambia Waandishi wa Habari usiku wa April 13, 2017 kwamba Kamati ilibaini ni kweli Kagera Sugar walifanya kosa hilo la kikanuni na adhabu yake ni kupokonywa ushindi.

Continue reading “KAMATI YA SAA 72 YAIPA SIMBA POINTI TATU KWA UZEMBE WA KAGERA SUGAR”

Sina chuki na Simba-Jerry Muro

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha klabu ya Yanga, Jerry Muro amesema wanaoamini kuwa ana chuki na uongozi wa klabu au mashabiki wa Simba wanajidanganya.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha klabu ya Yanga, Jerry Muro.

Muro amesema hayo siku moja tu baada ya kuhudhuria mazishi ya kiongozi wa zamani wa Simba, Said Pamba.

 

Muro alijumuika na wanachama na mashabiki wa Simba, akiwemo mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo, Hassan Dalali na Rais wa sasa, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’.

“Nilisisitiza toka mwanzo kuwa kuna maisha baada ya soka, kumbuka Yanga na Simba ni watani, kwenye utani wakati mwingine kuna maneno ya maudhi”

Aidha, Muro amesema hajawahi kuwa na chuki na Simba, lakini anataka Yanga ifanikiwe kwa kuwa yeye ni Yanga hata kabla ya kuwa kiongozi. Pia ameongeza kuwa ataendelea kuipigania klabu yake ya Yanga.

Jerry Muro amekuwa akionyesha kujiamini na kuwachanganya watu wa Simba kwa maneno yake ya kejeli ikiwa ni pamoja na kuwatungia majina ambayo yamekuwa maarufu.

Continue reading “Sina chuki na Simba-Jerry Muro”

Samatta aiongoza timu yake kucheza Europa

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta ameingoza KRC Genk kufuzu kucheza Ligi ya Europa baada ya kuichapa Sporting Charleroi kwa mabao 5­-1 na kushinda kwa jumla ya mabao 5-­3.

Royal Mouscron Peruwelz v KRC Genk - Jupiler Pro League
Samatta Mbwana Ally

Kulingana na gazeti la Mwananchi, Samatta, ambaye katika mchezo wa kwanza walionyukwa 2­0 alianzia benchi, jana aliaminiwa kuanza mchezo huo na kocha wake Peter Maes, akicheza pamoja na Nikos Karelis katika safu ya bora ya ushambuliaji. Continue reading “Samatta aiongoza timu yake kucheza Europa”

Harambee Stars yajiandaa kucheza na Taifa Stars

Timu ya taifa ya soka ya Kenya harambee stars imeanza kambi rasmi ya mazoezi mjini Nairobi zikiwa zimesalia siku chache kabla ya kucheza dhidi ya Tanzania katika mechi ya kirafiki.

160524135707_harambee_stars_camp_640x360_bbc

Wachezaji wa timu hiyo maarufu kama Harambee Stars wakiongozwa na kocha Stanley Okumbi walikusanyika uwanjani Kasarani na kufanya mazoezi ya kwanza Jumanne asubuhi. Continue reading “Harambee Stars yajiandaa kucheza na Taifa Stars”