Wema Sepetu na Diamond kunani ? Wema aweka video akiimba wimbo mpya wa Diamond ‘Utanipenda?’

Mpenzi wa zamani wa Diamond Platnumz, Wema sepetu ni shabiki mkubwa wa wimbo mpya wa msanii huyo ‘Utanipenda’

Screenshot_2015-12-15-05-31-28

Kwenye kipande kifupi cha video kilichowekwa kwenye snapchat ya rafiki kipenzi cha Wema sepetu, Aunty Ezekiel kimeowaoneshwa kwa pamoja wakiimba nyimbo hiyo ambayo imetoka siku tatu zilizopita, Wema na yeye kwenye Snapchat yake aliweka video ya bila sauti huku akiipa Caption ya ‘Je utanipendaga?’ ambayo ni jina la wimbo huo.

Siku chache zilizopita Wema sepetu alionekana akiwa karibu tena na ndugu wa mpenzi wake huyo wa zamani ambaye wana tabia ya kurudiana na kuachana, Romy Jones.

Credits: teamtz