USAIN BOLT BINGWA WA DUNIA MITA 200

Mwanariadha wa Jamaica Usain Bolt, ameshinda medali yake ya pili ya dhahabu, katika mashindano ya riadha ya dunia yanayoendelea mjini Beijing nchini Uchina.

 150823161129_usain_bolt_512x288_epa_nocredit

Bolt alitimuka mbio hizo kwa muda wa sekunde 19.55 na kunyakulia taifa lake medali nyingine mbali na kuandikisha rekodi ya kuwa mwanariadha kasi zaidi duniani katika mbio za masafa mafupi.

Ushindi huo ni wa kumi kwa mwanariadha huyo kutoka Jamaica na ni ya nne mfululizo katika mbio hizo za dunia.

 150823135550_justin_gatlin_624x351_reuters

Justin Gatlin wa Marekani, pia alishinda medali ya fedha katika mbio za mita mia moja, alimaliza wa pili akifuatwa na

Gatlin alitumia sekunde 19.74.

Katika fainali za mita mia nne kwa kina dada Felix Allyson wa Marekani alinyakuwa medali ya dhahabu, huku Shaunae Miller wa Bahamas akiridhika na medali ya fedha.

Shericka Jackson wa Jamaica naye alizoa medali ya shaba kwa kutumia muda wa sekunde 49.99.

Bingwa wa dunia wa mbio mita mia nane kwa kina dada, Mkenya Eunice Sum, nusura ayaage mashindano hayo pale alipomaliza katika nafasi ya tatu kwenye mbio za mchujo.

Hata hivyo Sum, alinusurika pale muda wake wa dakika 1.57.56 ulikuwa wa kasi zaidi kati ya wale waliomaliza katika nafasi ya tatu katika makundi yao, na hivyo kufuzu kwa fainali.

Advertisements

ARSENAL, BAYERN WAPANGWA KUNDI MOJA UEFA

Baada ya jana kufanyika droo ya makundi ya klabu bingwa barani Ulaya, mashabiki wa soka watapata fursa ya kushuhudia baadhi ya historia zikijirudia huku zingine mpya zikiandikwa.

 140220043435_arsenal_bayern_munich_512x288_afp_nocredit

Arsenal kwa mara ya tatu katika misimu minne, itavaana na Bayern Munich baada ya kupangwa kundi moja.

Wakati hayo yakijiri, mchezaji mpya wa Manchester Utd Memphis Depay atapata fursa ya kupambana na timu yake ya awali ya PSV Eindhoven ya uholanzi baada ya timu hizo kupangwa kundi moja.

Na ligi kuu ya Hispania La liga, pia mwaka huu imeweka historia baada ya mwaka huu kuingiza timu tano katika hatua hiyo ya makundi, jambo ambalo halikuwahi kutokea hapo awali.

Timu hizo ni Real Madrid, Barcelona, Atletico Madrid, Valencia pamoja na Sevilla.

MAMIA WAHOFIA KUZAMA MAJINI LIBYA

Zoezi la uokoaji zinaendelea katika pwani ya Libya baada ya boti mbili zilizokuwa na zaidi ya wahamiaji 500 kuzama karibu na bandari ya Zuwara.

 BBmaEcK

Watu zaidi ya ishirini na moja wameokolewa lakini mamia ya watu hawajulikani walipo wakihofiwa kufariki dunia.

Taarifa ambazo hazijathibitishwa zinasema kuna zaidi ya miili miamoja katika hospitali ya Zuwara, wakiwemo raia wa Syria, Bangaladesh na nchi kadhaa za Afrika katika jangwa la Sahara.

 BBmaM25

Hadi sasa kwa mwaka huu pekee,zaidi ya wahamiaji elfu mbili wamefariki wakijaribu kuvuka kutoka Libya kwenda Italia kwa boti ambazo sio salama ndani ya maji.

BBmaEun

WALIOFARIKI KWA KIPINDUPINDU KINONDONI WAFIKIA WATANO.

Idadi ya vifo vilivyosababishwa na ugonjwa wa kipindupindu katika Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam imeongezeka na kufikia watano baada ya hii leo watoto wawili kufariki dunia kwa ugonjwa huo.

kipindupindu-1

Idadi ya vifo vilivyosababishwa na ugonjwa wa kipindupindu katika manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam imeongezeka na kufikia watano baada ya hii leo watoto wawili kufariki dunia kwa ugonjwa huo.

Akiongea leo East Africa Radio Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dkt. Azizi Msuya amesema kuwa idadi ya wagonjwa imeendelea kuongezeka kutoka 52 hapo jana na kufikia 58 kutokana na wananchi kutozingatia maagizo wanayopewa na madaktari ili kuhakikisha ugonjwa hauendelei kuwaambukiza watu wengine.

Aidha, Dkt. Aziz amesema wagonjwa wanaongezeka wanatoka katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Kinondoni ikiwa ni pamoja na maeneo mapya yaliyopata maambukizi na sasa wamefikia wagonjwa zaidi ya 100 waliopokelewa na kutibiwa hadi sasa.

Chanzo: eatv.tv

WEMA SEPETU NA MAIMARTHA JESSE KIMEWAKA!!!

KUMEKUCHA! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema kufuatia mtifuano kati ya mtangazaji maarufu wa televisheni, Maimartha Jesse na staa wa filamu, Wema Sepetu baada ya bifu la wawili hao kufika jeshi la polisi.

WEMA_SEPETU06613

Akipiga stori na gazeti hili, Maimartha alisema Wema alikuwa na nia ya kumdhalilisha kwani baada ya kumtafuta na polisi na kumkosa, waliamua kumpigia simu na kumuita kituoni Kijitonyama (Mabatini) ambako alisomewa mashtaka ya kumtukana Wema katika mtandao wa kijamii wa Instagram.

Yaani Wema alitaka kunidhalilisha ndiyo maana polisi walikuja kibao kwenye gari lao hapa dukani kwangu na waliponikosa ndiyo wakanipigia simu kwamba niende mwenyewe kituoni, nikaenda nikatoa maelezo yangu ila sasa nitakula naye sahani moja kwani watu wake wanaendelea kunitukana sana mtandaoni nami siwezi kukubali,” alisema Maimartha.

Chanzo: GPL

LUNDENGA ASTAAFU, JOKATE AULA KAMATI YA MISS TANZANIA

Mwenyekiti wa kampuni ya lino wa international agency limited ambayo inahusika na kuandaa, na kuratbu pamoja na kusimamia mashindano ya urembo na umiss tanzania hashim lundenga amestaafu wadhifa wake.

r_5

akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, lundenga amesema amechukua uamuzi huo ilikutoa fursa kwa wengine kuchukua nafasi hiyo kutokana na kutumikia wadhifa huo kwa miaka 21.

katika tukio hilo, lundenga ameitaja kamati mpya ya Miss Tanzania ambapo nafasi yake ya uenyekiti ikichukuliwa na Juma Pinto huku makamu mwenyekiti Lucas Rutta, katibu mkuu Doris Mollel na msemaji wa kamati ni Jokate Mwegelo pamoja na wajumbe wapya nane.

“Mimi kama mkurugenzi pamoja na wenzangu tunabaki kuwa wamiliki wa kampuni na kuangalia hii kamati kile inachokifanya na zoezi hili sio la moja kwa moja bali ni la muda na mtu yeyote anaweza kufukuzwa kama atafanya kosa ama kuvunja mwiko wetu mkubwa ni kuhusu hawa washiriki ambao ni wasichana pia mtu yupo tayari kufanya chochote endapo akisikia kama kuna gari ama kitu cha thamani hivyo jambo hilo halifa vumiliwa” alisema

Huku Jokate Mwegelo ambaye ni msemaji wa kampuni hiyo wasichana ambao wamepoteza imani kutokana na matukio mbalimbali yaliyojitokeza hivi karibuni watarajie muonekano mpya kwani watarajie muonekano mpya wa mashindano hayo kwani watafanya kuwa bora kwa kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa na BASATA.

Dauka Somba

MAN U YASONGA MBELE UEFA

Katika muendelezo wa mechi za mkondo wa pili kufuzu kwenye mashindano ya klabu bingwa barani Ulaya, usiku wa kuamkia leo timu kadhaa zilishuka dimbani kutafuta tiketi ya kuingia katika hatua ya makundi.

 150808122844_manchester_united_1-0_tottenham_hotspur_624x351_bbc_nocredit

Manchester Utd imefanikiwa kusonga mbele kwa kishindo baada ya kuibuka na ushindi wa bao 4-0 dhidi ya Club Brugge na kufanya matokeo kuwa 7-1, katika mikondo yote miwili.

Katika mchezo huo nahodha Wayne Rooney alidhihirisha kuwa bado yupo vizuri katika kucheka na nyavu, baada kufunga mara tatu.

Droo ya makundi ya ligi hiyo, inatarajiwa kufanyika leo hii.

NUH MZIWANDA AENDELEA KUMKANA WEMA SEPETU

Msanii wa Bongo Fleva,Nuh Mziwanda amemkana tena staa wa Bongo Movie,Wema Sepetu kuwa hajawahi kumtongoza na sauti iliyorekodiwa kwenye simu akimtongoza mwigizaji huyo siyo yake.

NUH-MZIWANDA

Akizungumza kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM,alipokuwa akiachia ngoma yake mpya iitwayo ‘Hadithi’ alisema kuwa Wema hakuwa na nia nzuri na penzi lake na Shilole na alitaka kuwagombanisha na mpenzi wake huyo.

Sijawahi kumtongoza Wema na hakuwa na nia nzuri na penzi langu na Shilole alitaka kutugombanisha na nasisitiza ile sauti haikuwa yangu,’’alisema Nuh Mziwanda.

cloudsfm.com

RAY ASHUSHA KILIO UKUMBINI

Msanii wa filamu Vicent Kigosi ‘Ray’ hivi karibuni alijikuta akiangua kilio ukumbini baada ya mshindi wa shindano la kusaka vipaji vya kuigiza kufananishwa na marehemu Steven Kanumba.

ray267

Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Posta, jijini Dar kulipokuwa na fainali za Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) ambapo washiriki 10 ndiyo walikuwa wakiwania kitita cha shilingi milioni 50.

Mara baada ya mshindi wa shindano hilo kutangazwa, ukumbi mzima ulizizima kwa kelele za furaha na kwenda kumpongeza Dennis Laswai aliyeibuka kidedea na wengi walikubaliana kuwa ni haki yake kutokana na kufanya vizuri.

Wakati mshindi na mashabiki wake wakiendelea kufurahia ushindi, kundi la vijana lilipanda jukwaani wakiwa wameshika fulana yenye picha ya marehemu Kanumba huku wakisema mrithi wake amepatikana.

ray245

Ndipo ghafla, Ray ambaye alikuwa na upinzani wa kisanii na muigizaji huyo, alipoanza kumwaga machozi hadharani na kujikuta amezungukwa na watu wakimshangaa.

“Jamani mrithi wa Kanumba amepatikana rasmi baada ya miaka mitatu kuishi bila yeye, sasa jembe limerejea tena, mama yetu hapaswi kuwa na simanzi kila siku,” kijana mmoja alisikika akisema huku akienda kumshika mkono mama Kanumba.

Hali ilikuwa mbaya zaidi kwa Ray baada ya mmoja wa vijana hao kumfuata na kumuonesha fulana hiyo ambapo alizidisha kilio kiasi cha wenzake kumfuata na kumtuliza ili awe katika hali ya kawaida.

Mtu mmoja ukumbini hapo alibeza kilio hicho, akisema hiyo yote ilitokana na kuzidisha ‘kiburudisho’ na wala haikuwa kwa sababu ya kummiss sana marehemu kwani hawakuwahi kuwa na ukaribu wa kiwango hicho.

“Ray hana lolote, pale amezidisha kiburudisho tu, hakuwa na mapenzi na Kanumba kiasi hicho mpaka leo hii alie vile, ni usanii tu hakuna lolote. Wapo watu wa kulizwa na kitu kama kile na si yeye, halafu Ray huwa hana ushirikiano mzuri na wasanii wenzie hasa wa kiume,” alisema mtu huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake.

ray22

Kwa upande wake Ray alisema kilichomtoa machozi ni ukweli kwamba mshindi ana kipaji cha hali ya juu na yeye binafsi alipenda ushindi wake kiasi kwamba mawazo yake yalimfikisha mbali.

Imeandaliwa na Shani Ramadhani, Mayasa Mariwata na Musa Mateja.

Chanzo: GPL

News, Entertainment, Sports, Music, Videos, Current Affair, Lifestyle, and Gossip.