VIJANA WAUZA TAMTHILIA NA FILAMU ZA NJE WAANDAMANA KUIOMBA SERIKALI KUWARUHUSU WAUZE CD HIZO.

WAFANYABIASHARA wadogo wadogo ‘Machinga’ wanaouza filamu za kigeni wameandamana wakiomba kukutana na Rais Dr John Magufuli ili kusikilizwa juu ya kupigwa marufuku kuuza filamu hizo hapa nchini.

Marufuku hiyo ilitolewa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Harrison Mwakyembe, siku chache baada ya kuteuliwa katika nafasi hiyo mara baada ya kukutana na waigizaji wa ndani ambapo walieleza malalamiko yao juu ya filamu za nje kuharibu soko la kazi zao. Continue reading “VIJANA WAUZA TAMTHILIA NA FILAMU ZA NJE WAANDAMANA KUIOMBA SERIKALI KUWARUHUSU WAUZE CD HIZO.”

SHERIA ISEMAVYO KUHUSU HAKI NA WAJIBU WA MMILIKI ARDHI, NA GHARAMA ZA KUKIUKA SHERIA ZA UMILIKI”

Mwanasheria; Rachel Kilasi – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , akifafanua sheria ya Ardhi na. 4 ya mwaka 1999 sambamba na Umiliki wa Ardhi (Haki, Wajibu na uzingatiaji wa ulipaji wa Pango la Kodi ya Ardhi kwa Mmiliki).
unnamed.png
………………..
Mwananchi yoyote ana haki ya kupatiwa Hatimiliki ambayo ni nyaraka halali ya umiliki wa ardhi baada ya kupata ridhaa ya Kamishna au Kamati na kulipa ada stahili. Hatimiliki hutolewa ndani ya siku 90 mpaka 180 baada ya ridhaa husika.

Continue reading “SHERIA ISEMAVYO KUHUSU HAKI NA WAJIBU WA MMILIKI ARDHI, NA GHARAMA ZA KUKIUKA SHERIA ZA UMILIKI””

KAMATI YA SAA 72 YAIPA SIMBA POINTI TATU KWA UZEMBE WA KAGERA SUGAR

Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi Tanzania, maarufu kama Kamati ya Saa 72 imeipa Simba SC pointi tatu na mabao matatu kutokana na rufaa waliyoikatia Kagera Sugar kwa kumtumia beki Mohammed Fakhi akiwa ana kadi tatu za njano katika mechi baina ya timu hizo Aprili 2, mwaka huu.
IMG-20170413-WA0104-640x427.jpg
Katika mchezo huo ambao Kagera Sugar walishinda mabao 2-1 Uwanja wa Kaitaba, wanadaiwa kukiuka kanuni kwa kumchezesha Fakhi, beki wa zamani wa Simba badala ya mchezaji huyo kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano alizopata mfululizo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Ahmed Yahya amewaambia Waandishi wa Habari usiku wa April 13, 2017 kwamba Kamati ilibaini ni kweli Kagera Sugar walifanya kosa hilo la kikanuni na adhabu yake ni kupokonywa ushindi.

Continue reading “KAMATI YA SAA 72 YAIPA SIMBA POINTI TATU KWA UZEMBE WA KAGERA SUGAR”

Dk Wilson Ngwale Apewa Uwenyekiti Bodi ya TBA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Waziri wa Ujenzi, Uchukukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mnyaa Mbarawa (Mb), kwa mamlaka aliyopewa kwa mujibu wa Sheria ya Wakala wa Serikali Na. 30 ya mwaka 1997 pamoja na marekebisho yake kupitia Sheria Na. 13 ya mwaka 2009 amemteua Dkt. Edward Wilson Ngwale kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe 10.04.2017.

Mh. Prof. Makame Mnyaa Mbarawa.

Mhe. Prof. Mbarawa amemteua Dkt. Ngwale kushika nafasi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka mitatu katika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi baada ya uteuzi wa awali kufika ukomo.
Aidha, sambamba na uteuzi huo Prof. Mbarawa amewateua Wajumbe watano (5) wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Majengo Tanzania kuanzia tarehe 10.04.2017 kama ifuatavyo:-
1. Eng. John Bura – Mkandarasi kupitia Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB)
2. Arch. Pius P. Tesha – Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
3. Prof. Bakari M. M. Mwinyiwiwa – Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
4. Bw. Ntuli Lutengano Mwakahesya – Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
5. Eng. Amiri N. Mcharo – Wizara ya Fedha na Mipango.

Imetolewa na;

Eng. Joseph M. Nyamhanga
KATIBU MKUU (UJENZI)
12.04.2017

Manji, Mbowe, Gwajima na Azzan Watajwa na Makonda Orodha ya Dawa za Kulevya

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam ameendelea kutingisha vyombo vya habari baada ya leo kuibuka na majina mengine 65 ya watuhumiwa wa dawa za kulevya. Katika orodha hiyo mpya yumo tajiri maarufu Yusuf Manji, aliyekuwa Mbunge wa Kinondoni, Idd Azzan Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe pamoja na Mchungaji maarufu Gwajima.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisi kwake leo jijini Dar, Makonda alisema watuhumiwa wote hao watatakiwa kufika Kituo cha Kati cha Polisi siku ya Ijumaa majira ya saa tano asubuhi kwa mahojiano zaidi. Aidha Makonda amekiri kukamatwa kwa Mmiliki wa kituo cha Radio ya EFM, Francis Ciza, almaarufu kwa jina la Dj Majay kwa tuhuma hizo. “Tulipokuwa tukifanya oparesheni ya kuwakamata wahusika wote wa dawa za kulevya juzi usiku naye akakamatwa kwa mahojiano zaidi,” alisema Mkuu wa Mkoa Makonda. Continue reading “Manji, Mbowe, Gwajima na Azzan Watajwa na Makonda Orodha ya Dawa za Kulevya”

Mahakama Zamkera JPM, ni Kuhusu Kesi za Ukwepaji wa Kodi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akihutubia wakati  wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akihutubia wakati
wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017

Mahakama Zamkera JPM, ni Kuhusu Kesi za Ukwepaji wa Kodi

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameelezea kusikitishwa kwake na namna Mahakama inavyoshughulikia kesi zinazohusiana na ukwepaji wa kodi na ametoa wito kwa mahakama na wadau wake kujipanga kukabiliana na dosari hiyo inayorudisha nyuma juhudi za maendeleo ya nchi. Continue reading “Mahakama Zamkera JPM, ni Kuhusu Kesi za Ukwepaji wa Kodi”

Mwongozo Mpango wa Ujenzi wa Barabara Wazinduliwa

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamuhanga (kushoto), akikata utepe kwenye kitabu cha Mwongozo wa ujenzi wa Barabara zinazotumiwa na magari machache, mara baada ya kuuzindua leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Meneja wa AFCAP Kanda ya Mashariki na Kati mwa Afrika, Eng. Nkulule Kaleta.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamuhanga (kushoto), akikata utepe kwenye kitabu cha Mwongozo wa ujenzi wa Barabara zinazotumiwa na magari machache, mara baada ya kuuzindua leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Meneja wa AFCAP Kanda ya Mashariki na Kati mwa Afrika, Eng. Nkulule Kaleta.

SERIKALI imezindua mwongozo wa mpango na usanifu wa ujenzi wa barabara zinazopitisha magari machache kwa lengo la kutoa maelekezo na kuwawezesha wahandisi wanaofanya usanifu wa barabara hizo kutumia gharama nafuu za ujenzi.
Akizungumza katika uzinduzi huo leo jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga amesema kuwa mwongozo huu utakuwa tiba na kuwezesha Serikali kujenga barabara nyingi na gharama nafuu. Continue reading “Mwongozo Mpango wa Ujenzi wa Barabara Wazinduliwa”

Rais Magufuli Amteuwa Jenerali Venance Mabeyo Mkuu wa Majeshi Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Luteni Jenerali Venance Salvatory Mabeyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Luteni Jenerali Venance Salvatory Mabeyo.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli, leo Tarehe 02 Februari, 2017 amemteua Luteni Jenerali Venance S. Mabeyo kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania. Continue reading “Rais Magufuli Amteuwa Jenerali Venance Mabeyo Mkuu wa Majeshi Tanzania”