TUZO ZA FILAMU TANZANIA 2015 ZAINGIA KWENYE HATUA YA MWISHO!

TAFA-2-532

Mkutano na waandishi wa habari shirikisho la filamu Tanzania pamoja na wadau na waandaji wa tuzo hizo, wameonyesha furaha kubwa kwa hatua waliyofikia hadi sasa. Tuzo za filamu Tanzania chini ya shirikisho la filamu ndizo Tuzo zenye hadhi ya juu kabisa katika tasnia hii. Tuzo hizi zilizozinduliwa rasmi mwaka jana mwezi wa kumi na moja zimeonyesha mwamko mkubwa sana katika uchukuaji na urekeshaji wa fomu na hatimaye kufikia hatua hii ya kuwapata, NOMINEES.Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Simon Mwakifwamba akielezea jambo kwa wana habari(hawapo pichani) wakati wa kutangaza walioingia katika hatua ya mwisho ya kushindania Tuzo za Filamu Tanzania leo jijini Dar es Salaam katika mkutano na wana habari uliofanyika katika hotel ya New Africa ya jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tuzo hizo Caroline Gul na mmoja wa wadhani kutoka International Eye Hospital Dr. Recep Yujel.

Advertisements

SUMA LEE MUZIKI BASI

Sumalee_full (1)
Msanii aliyefanya vizuri na single ya ‘Hakunaga’, Suma Lee amesema hatofanya tena muziki kwa sababu ameachana kabisa na maisha hayo.

Suma ambaye alitengeneza pesa nyingi kupitia hit yake ya ‘Hakunaga’, amesema hana mpango wa kuzitoa nyimbo zake zilizoko studio ambazo hazijatoka.

“Sifanyi tena muziki na nimeachana kabisa na maisha hayo, na nyimbo zote zilizobaki studio nimezisimamisha zisitoke baada ya kuzilipia, “ Alisema Suma.

“Kuna wimbo mmoja nimefanya na Cp ambao ndio ulikuwa wa kurudisha kundi la Parklane, pia nimeuzuia, labda Cp auchukue yeye.

Kilichobaki ni kuwaombea wazazi wetu waliotutangulia, wengine walikuwa hawata ki tufanye kazi hizi, kwa kuwa hawapo na hakuna wakutukataza tena, bora tukae na kuwaombea.”

TAARIFA KUHUSU ASKARI KUUAWA

10338338_1186168991397517_1276094659587300095_n

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Polisi Mkoa wa Pwani linaendesha oparesheni kali ya aina yake ya kuwasaka watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi waliowavamia, kuwauwa askari wawili na kumjeruhi mmoja na kisha kupora bunduki aina ya SMG.
Tukio hilo limetokea tarehe 30/03/2015 majira ya saa mbili usiku huko barabara ya Kilwa Kata ya Vikindu Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani. Katika tukio hilo majambazi wapatao 8 hadi 10 wakiwa na mapanga na silaha zingine waliwavamia ghafla askari watatu waliokuwa kazini katika eneo la kizuizi cha Polisi kilichopo kijiji cha Kipara mpakani Kata ya Vikindu Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani. Majambazi hao wakiwashambulia ghafla askari hao kisha kupora silaha aina ya SMG ikiwa na risasi 30 ndani ya magazine na kutokomea kusikojulikana.
Majina ya askari wa Wilala ya Kipolisi ya Mbagala waliouawa ni kama ifuatavyo:
D.2865 SGT FRANCIS,
E.177 CPL MICHAEL,

Karibu Hapa

Naitwa Alli Matala,ni kijana wa makamo ambaye ni raia wa Tanzania mwenye Elimu ya uhandishi wa habari na utangazaji wa radio na Television.

Nimatumaini yangu kuwa hu mzima bukheri wa afya Njema na unaendelea vyeama katika harakati za kulijenga Taifa,Ningependa kuchukua nafasi hii kukukaribisha katika Blogu yangu ambayo nimeipatia jina la HabariZao,

Nimeamua kufungua blogu hii kwa si kwakuwa mimi ni muhandishi wa habari pekee na mtangazaji La asha kwa kuwa sasa Jamii imekuwa kama aielewi nini maana ya Tasnia hii na kumeibuka utitiri wa vyombo vingi vya habari lakini sio vyenye kuzingatia maadili ya uhandishi wa habari.

wengi wao ni wavivu wa kufikiri na kuchapa kazi ndio maana nimeona nifungue blogu hii labda itakuwa fundisho kwao,habari nyingi kwa sasa kuanzia kwenye radio,blogu, na hata kwenye televison hapa Tanzania zimekuwa ni za kufanana sana  utapita katika vyombo vyote vya habari hapa Tanzania utakuta habari ni zile zile zikijirudia tena kwa muundo wa kukopi na kupesti bila hata haya.

blogu hii itajihusisha na habari za Burudani za nje na ndani ya tanzania, Michezo, Uchumi, siasa, utamaduni, biashara na hata kilimo ili kuwapa fursa wasomaji wote waweze kupata habari zote bila ya kuhangahika kuperuzi na mitandao mingine..

ningependa kukuarika msomaji wangu tuwe pamoja kuanzia leo hii hadi mwisho wa uhai wa blogu hii.

pia niwajibu wako kuchangia habari yoyote ile na kushare popote pale bila ya kuathiri kazi hiyo na kutumia lugha za kistaarabu bila matausi karibu sana100_3157

News, Entertainment, Sports, Music, Videos, Current Affair, Lifestyle, and Gossip.