Tag Archives: FIFA

FIFA kufanya mabadiliko ‘World Cup’ haraka

Rais wa shirikisho la soka la kimataifa Gianni Infantino ameunga mkono mapendekezo yaliyyotolewa na shirikisho la soka la bara la America Kusini (CONMEBOL) la kuongeza timu 16 kwenye fainali za Kombe la dunia 2022.

Continue reading FIFA kufanya mabadiliko ‘World Cup’ haraka

Advertisements

ORODHA YA NCHI ZITAKAZOTEMBELEWA NA KOMBE LA DUNIA

Wakenya wamejitokeza kwa wingi kulitazama na kupigwa picha na Kombe la Dunia la Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) ambalo limekuwa nchini humo kwa siku mbili.

Kombe hilo ambalo liliwasili nchini Kenya na kupokelewa na Rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta lilipata watazamaji wengi ambao walifika kujionea na kupiga picha pamoja na kombe hilo. Continue reading ORODHA YA NCHI ZITAKAZOTEMBELEWA NA KOMBE LA DUNIA

Sepp Blatter: Nitawasilisha rufaa

Mwanasheria wa aliyekuwa Rais wa shirikisho la Soka Duniani FIFA Sepp Blatter anatarajiwa kuwasilisha rufaa yake kupinga kufungiwa miaka minane kujishughulisha na masuala ya soka.

 151221112349_blatter_512x288__nocredit

Hata hivyo kamati ya nidhamu ya FIFA imewasilisha sababu za kuchukuliwa kwa hatua za nidhamu dhidi ya viongozi hao waandamizi wa zamani wa soka Blatter na mwenzake, Michel Platini. Mwezi Disemba aliyekuwa Rais wa FIFA Sepp Blatter na rais wa UEFA Michel Platini walifungia kwa kipindi cha miaka minane baada ya kukutwa na hatia ya kuvunja kanuni na sharia za FIFA. Kwa upande wake pia mwanasheria wa Platini anasema kuwa anatarajia kukata rufaa kwa kupinga maamuzi ya FIFA.

Chanzo:bbcswahili.com

Blatter alazwa kwa kupata mshituko

Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa, Sepp Blatter amelazwa hospitalini kutokana na kupatwa mshituko wa neva.

150530094921_deportes_futbol_blatter_fifa_624x351_pa

Blatter aliyesimamishwa kwa siku 90 kujishughulisha na masuala ya soka wakati akichunguzwa kwa kashfa za rushwa , alilazwa hospitalini kwa ajili ya uchunguzi wa afya lakini sasa imeelezwa ataendelea kubaki huko.

Mwanamichezo huyo aliyeongoza ulimwengu wa soka kwa miaka 18 mpaka sasa, awali ilidaiwa alikuwa na matatizo ya msongo wa mawazo hivyo ikabidi apate huduma ya matabibu, sasa imebainika ana tatizo la mshituko wa neva.

Awali, mwanasheria wake, Richard Cullen alieleza juu ya uangalizi huo wa madaktari kutarajiwa, lakini akasema alitarajia arejee nyumbani mapema kabla hali kubadilika na kutolewa maelezo tofauti.

Hata hivyo, watu wake wa karibu wameeleza hali yake si mbaya na anatarajiwa kurejea katika hali ya kawaida japokuwa atabaki hospitalini hadi mapema wiki ijayo.

Msaidizi wake, Walter Gagg, amesema kwamba bosi huyo anatarajiwa kuwa mwenyeji wa hafla ya kukabidhi tuzo ya Mwanasoka Bora hapo Januari 11 mwakani.

Chanzo: bbcswahili.com

Issa Hayatou achukua uongozi wa Fifa

Kiongozi wa shirikisho la soka barani Afrika Issa Hayatou kutoka Cameroon amepewa jukumu la kuongoza shirikisho la soka duniani Fifa kwa muda.

 141103144226_issa_hayatou_caf_512x288_afp

Hayatou atachukua usukani kufuatia kusimamishwa kazi kwa Rais wa Fifa Sepp Blatter kwa muda wa siku 90 na Kamati ya Maadili ya shirikisho hilo, shirikisho hilo linalosimamia soka duniani limesema kupitia taarifa.

Hayatou, aliyeongoza CAF tangu 1988, atachukua usukani kwa mujibu wa sheria za Fifa, akiwa ndiye makamu wa rais katika kamati tendaji ya Fifa aliyehudumu muda mrefu zaidi.

Baadaye, Hayatou ametoa taarifa na kusema amepokea majukumu hayo mapya lakini ataongoza tu kwa muda.

“Rais mpya atachaguliwa kwenye Mkutano Mkuu Februari 26, 2016. Na mimi mwenyewe sitawania,” amesema kupitia taarifa.

“Hadi mkutano huo ufanyike, naahidi kwamba nitajitolea kwa nguvu zangu zote kutumikia shirikisho hili, mashirikisho wanachama, waajiri wetu, washirika na mashabiki wa soka popote walipo.”

Aidha, ameahidi kuendelea kushirikiana na watawala na kuendeleza uchunguzi kwenye shirikisho hilo lililoyumbishwa na madai ya ulaji rushwa.

Fifa: Argentina katika viwango vya ubora duniani

Shirikisho la soka duniani Fifa limetangaza viwango vya ubora vya mchezo wa soka kwa mwezi Septemba ambapo taifa la Argentina limeendelea kuongoza katika chati hiyo.

 151001221607_fifa_argentina_640x360_bbc_nocredit

Mabingwa wa dunia Ujerumani wako nafasi ya pili, Ubelgiji wanashika nafasi ya tatu katika viwango vya ubora.

Algeria ndio taifa la Afrika linaloongoza likiwa nafasi ya 19 huku Ivory Coast wakiwa nafasi ya 21 .

Kwa upande wa Afrika mashariki Uganda wako juu wakiwa nafasi ya 75,Rwanda iko katika nafasi ya 93 huku Burundi wakijichimbia katika nafasi ya 113, kenya wao wako nafasi ya 131 na Tanzania ikiwa nafasi ya 136.

Orodha ya kumi bora

1 Argentina

2 Germany

3 Belgium

4 Portugal

5 Colombia

6 Spain

7 Brazil

8 Wales

9 Chile

10 England

FIFA:Blatter na Platini wachunguzwa

Rais wa FIFA Sepp Blatter na rais wa UEFA Michel Platini wanachunguzwa na kamati ya nidhamu ya FIFA.

 150925144933_blatter_platini_624x351_afp_nocredit

Haya yamewadia baada ya thibitisho kutoka kwa mwanasheria mkuu wa Switzerland kuwa ameanzisha uchunguzi dhidi ya wawili hao.

Blatter anakabiliwa na mashtaka mawili makuu,kutoa kandarasi ambazo zingeigharimu FIFA na kutoa malipo ya zaidi ya Franka milioni mbili za uswisi kwa rais wa UEFA Platini.

 150903024843_polica_vigila_la_fifa_en_zurich_624x351_getty_nocredit

Mawakili wa Blatter wamesema kuwa wao hawana wanaloficha na kuwa watashirikiana kikamilifu na afisi ya mkuu wa sharia.

Rais huyo wa FIFA amekanusha madai dhidi yake.

Platini -ambaye alikuwa ni mshauri wa kiufundi wa Blatter kati ya mwaka wa 1999 na 2002 anatarajiwa kutoa ushahidi dhidi yake.

Raia huyo wa Ufaransa ambaye anawania kumrithi Blatter amekanusha madai yanayomkabili ijapokuwa ameshindwa kueleza kikamilifu kwanini malipo hayo yamecheleweshwa kwa miaka tisa !

bbcswahili.com

Orodha ya viwango vya soka duniani, Argentina yaongoza

Shirikisho la Soka duniani Fifa imetoa orodha ya Ubora Duniani kwa mwezi wa Nane ambapo Argentina inaongoza ikiwa nafasi ya kwanza.

 150706170147_fifa_640x360_fifa

Ubelgiji wao wako katika nafasi ya pili huku mabingwa wa dunia Ujerumani wakiwa katia nafasi ya tatu.

Kwa Afrika, Nchi za juu kabisa ni zile zile na zimeshika Nafasi hizo hizo za Mwezi uliopita na hizo ni Algeria ambao wako Nafasi ya 19 wakifuaťiwa na Ivory Coast ambao ni wa 21.

Kwa nchi za ukanda wa afrika mashariki Uganda wanaongoza wakiwa nafasi ya 71,Rwanda wako nafasi ya 78, kenya wao wanashika nafasi ya 116, Burundi wao wako nafasi 134 huku Tanzania wakiwa nafasi ya 140.

Orodha ya ubora duniani

1 Argentina

2 Belgium

3 Germany

4 Colombia

5 Brazil

6 Portugal

7 Romania

8 Chile

9 Wales

10 England

HII NI RIPOTI YA ORODHA YA VIWANGO VYA UBORA WA SOKA DUNIANI

Shirikisho la mpira wa miguu duniani Fifa limetangaza ubora wa viwango kwa mwezi Agosti ambapo timu ya taifa ya Argentina imeendelea kushika nafasi ya kwanza.

 150529152513_fifa_logo_640x360_getty_nocredit

Ubelgiji imepanda kwa nafasi moja mpaka nafasi ya pili huku mabigwa wa dunia Ujerumani wakiwa katika nafasi ya tatu.

Timu ya juu kabisa toka Barani Afrika ni Algeria ambayo ipo pale pale Nafasi ya 19 na kufuatiwa na Ivory Coast waliobakia Nafasi ya 21.

Timu za ukanda wa Afrika mashariki zinaongozwa na Uganda walioko nafasi ya 74,Rwanda wakiwa katika nafasi ya 91 Kenya 116,Burundi wakishika nafasi ya 132 na Tanzania wakiwa latika nafasi ya 140

Ifuatayo ni listi ya timu kumi bora duniani kwa mwezi Agosti

  1. Argentina

  2. Belgium (Imepanda nafasi 1)

  3. Germany

  4. Colombia

  5. Brazil (Imepanda 1)

  6. Portugal (Imepanda 1)

  7. Romania (Imepanda 1)

  8. England (Imepanda 1)

  9. Wales (Imepanda 1)

  10. Chile (Imepanda 1)