Tag Archives: Global Peace Foundation

FORMER ZANZIBAR PRESIDENT KARUME, EAST AFRICA LEADERS TO CONVENE AT GREAT LAKES REGION PEACE AND DEVELOPMENT SUMMIT IN UGANDA

On the invitation of President of the Republic of Uganda, H.E Yoweri Museveni, Former Zanzibar President H.E Dr Amani Abeid Karume will join a delegation of East African leaders to explore regional peace and security issues and discuss innovative approaches that will improve economic opportunity, advance excellence and equality in education, increase youth productivity, support women’s empowerment, and address critical community development needs at a convening of regional leaders in Kampala of August 1-2, 2018. Continue reading FORMER ZANZIBAR PRESIDENT KARUME, EAST AFRICA LEADERS TO CONVENE AT GREAT LAKES REGION PEACE AND DEVELOPMENT SUMMIT IN UGANDA

Advertisements

Global peace foundation Tanzania: kumpa wanawake elimu bora ni kujenga jamii bora.

Katika kuelekea siku ya wanawake duniani Global Peace Foundation Tanzania wameendelea kampeni yao ya kuhamasisha amani duniani ambapo siku ya leo walikuwa wakiadhimisha siku hiyo katika shule ya sekondary ya St. Anne Marie Accademy ya jijini Dar es salaam. Continue reading Global peace foundation Tanzania: kumpa wanawake elimu bora ni kujenga jamii bora.

Global peace Foundation Tanzania: Yatoa mafunzo juu ya kujiepusha na kuingia katika makundi ya misimamo mikali.

 

Ikiwa ni muendelezo wa kutoa elimu kwa jamii leo global peace foundation Tanzania imeitaka jamii kuweka utaratibu wa kutatua migogoro ambayo inakuwepo ndani yake ili kuepusha ukosefu ama uvunjifu wa Amani.

wajumbe katika mafunzo wakiwa katika picha ya pamoja

Hayo yamezungumza na Godwin Mongi  kutoka baraza la taifa la dini mbalimbali katika kujenga Amani  akiwa anatoa mafunzo kwa walemavu  mbalimbali ambapo  elimu ilikuwa ikitolewa ya namna ya kuilinda na kudumisha Amani pamoja na ujasiriamali.

Godwin Mongi  kutoka baraza la taifa la dini mbalimbali katika kujenga Amani

Amesema makundi ambayo yanaweza kusababisha uvunjifu wa Amani ni pamoja na makundi ya misimamo mikali ya dini, siasa kali ufurutu, na ufuruta ada,  na kuzitaja sababu kuwa ni pamoja na ukandamizaji, ubinafsi, na ukosefu wa usawa, ushawishi wa viongozi wa kisiasa, dini.

IMG_0351
Mkurugenzi Mkaazi wa Gloabal peace Foundation Tanzania Bi. martha Nghambi akifuatilia kwa umakini mafunzo ambayo yalikuwa yakitolewa.

Na upande wa wajumbe ambao waliudhuria mafunzo hayo wametaja kuwa zipo sababu nyingine ambazo huwapelekea kuwa na misimamo mikali ambapo wamesema kuwa uongozi mbovu, matumizi mabaya ya madaraka tume za haki za binaadamu na utawala bora kutosimama vema kuwatetea walemavu.

Hata hivyo wamepongeza serikali, mashirika na taasisi zsizo za kiserikali kwa kuwapatia elimu ya kujitambua, biashara na uchumi, huku wakiitaka serikali isimamie kuwepo na mabaraza ya walemavu na kuanzia ngazi ya serikali ya mtaa kuwe na wawakilishi wa watu wenye ulemavu ili kuondoa dhana iliyopo sasa ya kuonekana wanatengwa.

Dickson Daniel kutoka Global peace Foundation Tanzania akitoa mafunzo ya butengenezaji wa sabuni ya maji.

Mbali na elimu hiyo ambayo imetolewa siku ya leo pia wamepata nafasi ya kufundishwa elimu ya ujasiriamali ambapo siku ya leo mafunzo ya kutengeneza sabuni na mkaarafiki yalitolewa kwa washiriki, Global peace foundation Tanzania itwakuwa ikiendelea kutoa elimu.

Picha zaidi.

 

Thamani ya Binti katika uongozi wa Maadili: Global Peace Foundation Tanzania

Kila ifikapo tarehe October 11, dunia inafanya maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani, ambapo siku ya leo Taasisi isiyo ya kiserikali Global peace Foundation Tanzania imeadhimisha siku hii katika shule ya sekondari Turiani iliyopo Kinondoni  jijini Dar es salaam.

 

IMG_9125

Huku Taasisi ya Global ikiongozwa na mkurugenzi mkaazi Martha Nghambi imetoa rai kwa kuwataka wanafunzi vijana wa kitanzania kuhakikisha amani wakihiubiri wakiwa nyumbani pia hata wawapo mashuleni mwao.

IMG_8982

Ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya vijana na amani ambayo yenye lengo la kuhakikisha amani inadumishwa duniani hasa katika taifa la Tanzania Bi Ng’abi amewasisitiza wanafunzi kuwa mabalozi wa kweli “Ukiona mama anapigwa ujue hapo hakuna amani, motto akichapwa hakuna amani hata nyanyasaji ukifanyika basi hakuna amani hivyo niwatake wanafunzi muwe chachu na mabalozi wazuri wa amani nyumbani na shuleni”. Alisema.

IMG_9190

Mgeni rasmi alikuwa katika maadhimisho alikuwa Jokate Mwegelo, amabye ni mwanamitindo na msanii pia ni mwanaharakati wa masuala ya mabinti ambaye ni mkurugenzi wa Kidoti Foundation, naye amewahasa mabiti mashuleni kuwa na nidhamu, Kujithamini, wajitambue,  utii, bidii pia na malengo katika kusaka Elimu yao.

IMG_9138

“Niwatake rai wanafunzi pindi mnapokuwa mashuleni mjithamini, mjitambue, mshiriki midahalo mbalimbali, mjiamini ili katika maisha yenu ya baadae yaweze kuwa mazuri Alisema. Huku akiongeza kuwa wajitunze na watoto wa kike wasitingishwe na mtu yeyote kwa kuambiwa kuwa hawawezi ama kukatishwa malengo yake kwa namna yoyote ile,

IMG_8941

Hilda Ngai  Mwanaharakati wa masula ya watoto wa kike (Mwanamke na Uongozi) amesema mabinti waweke nguvu zao katika masomo na uongozi na ndoto zao katika maisha yao. “Mwanamke ma motto wa kike unatakiwa ue na malengo lakini huwezi kufikia malengo hayo kama hutoweka nguvu katika ndoto zako za baadae”. Alisema.

IMG_9215

Maadhimisho ya Siku ya motto wa kike duniani ufanyika kila oktoba 11 na Ujumbe kwa mabinti katika maadhimisho hayo ni “Thamani ya Binti katika uongozi wa Maadili”. Takwimu zinaonyesha kuwa kila palipo na mabinti kumi kuna uwezekano mabinti watatu kuna uwezekano wa kupata mimba hivyo jamii isimame katika kupambana kumpatia ulinzi na uwezo motto wa kike ili aweze kutimiza malengo yake.

IMG_9249IMG_9317IMG_9170IMG_8961IMG_8943IMG_8953

Global Peace Foundation Tanzania: Vijana baada ya shule waepuke uvunjifu wa amani.

Taasisi ya Global peace Foundation Tanzania imewataka vijana wa kitanzania kushiriki katika kulijenga taifa pindi wanapohitimu masomo yao wakiwa shule na vyuoni ili kuepuka kujiingiza katika matukio ya uvunjifu wa amani.

Continue reading Global Peace Foundation Tanzania: Vijana baada ya shule waepuke uvunjifu wa amani.

Global Peace Foundation Tanzania: wazazi jengeni mahusiano mazuri kuleta amani.

Wazazi wa kitanzania wametakiwa kujenga misingi malezi bora ya malezi ili kuleta amani ndani na nje ya familia.

img_1306

Akizungumza mapema leo katika mjadala ambao umefanyika katika zahanati ya Tandale jijini Dar es salaam mkurugenzi mkazi wa Global Peace Foundation Tanzania Martha Nghambi amesema kuwa wazazi ni lazima washiriki kikamilifu katika kujenga misingi ya malezi. Continue reading Global Peace Foundation Tanzania: wazazi jengeni mahusiano mazuri kuleta amani.

Global Peace Foundation Tanzania yawasihi vijana kulinda amani

Shirika la Global Peace Foundation Tanzania limewataka vijana kushiriki kikamilifu katika kuilinda na kuwa chanzo cha Amani katika nchi ya Tanzania.

_DSC0890

Hayo yamezungumza na Martha Nghambi, Mkurugenzi Mkazi jana katika kituo cha afya cha Tandale ambapo kulikuwa na warsha ambayo iliandaliwa na Global Peace Foundation pamoja na Tandale Youth Development Center huku akisisitiza kama vijana ambao wanatarajia kuwa wazazi wa baadae wawe mifano ya kuigwa. Continue reading Global Peace Foundation Tanzania yawasihi vijana kulinda amani

GLOBAL PEACE FOUNDATION TEACHES CHILDREN TO LOVE EACH OTHER, AS WE ARE ALL ONE FAMILY UNDER GOD.

Global Peace Foundation –Tanzania with its headquarters in America and having 20 branches worldwide reached a height in its efforts by educating pre-primary school from Crystal Wonderland located in Sinza, Dar es Salaam over the importance of living in peace and preserving harmony in their daily lives.
IMG_1935
The visit to the school is part of the organization’s initiative campaign known as “Vijana Na Amani” means ‘Youth and Peace’ which aims to educate and creating awareness to children and youths in safeguarding and preserving Tanzanian peace. Continue reading GLOBAL PEACE FOUNDATION TEACHES CHILDREN TO LOVE EACH OTHER, AS WE ARE ALL ONE FAMILY UNDER GOD.

Gloabal peace Foundation Tanzania yafundisha watoto kuishi kwa amani

Shirika ambalo si la kiserikali Global Peace Foundation Tanzania lenye makao yake nchini marekani na lenye matawi zaidi ya 20 duniani leo lilitembelea katikaShule ya awali Crystal Wonderland iliyopo Sinza Dar es salaam katika muendelezo wa kampeni ya ‘vijana na amani’ na kutoa elimu kwa watoto jinsi ya Kuishi vema ili kuilinda na kuidumisha ‪‎amani ya Tanzania.

IMG-20160530-WA0001

Katika ziara hiyo mkurugenzi mkazi wa Global Peace foundation Martha Nghambi amesema kuwa wameamua siku ya leo kutembele shule hiyo kwa kuwa utoto ni mwanzo wa Ujana, kumjengea Mtoto Utamaduni wa kupenda amani ni kumuandaa kuwa Balozi wa amani pindi atakapo kuwa mkubwa ni jambo la muhimu sana. Aliendelea pia na kutoa mfano wa msemo maarufu usemao “Samaki mkunje angali mbichi”. Continue reading Gloabal peace Foundation Tanzania yafundisha watoto kuishi kwa amani

Global Peace Foundation Tanzani yalaani mauaji yanayoendelea nchini.

Taasisi isiyo ya kiserikali Global Peace Foundation Tanzania kwa kushirikiana na wadau wa Amani nchini wanalaani vikali na kupinga vitendo vyovyote vya uvunjifu wa Amani nchini vinavyopelekea uhalifu dhidi ya maisha ya binadamu na ustawi wa maisha yao.

Global-Peace-Foundation-Logo2

Akizungumza na wanahabari mkurugenzi mkazi wa global peace foundation tanzani Martha nghambi amesema kuwa hivi karibuni kumeripotiwa na vyombo vya habari kuwepo kwa matukio kadhaa ya mauaji ya binadamu likiwamo tukio la mauaji ya wanafamilia saba na tukio la shinyanga la mauaji ya watu watatu katika msikiti wa Rahman mkoani mwanza. Continue reading Global Peace Foundation Tanzani yalaani mauaji yanayoendelea nchini.