Mahakama Zamkera JPM, ni Kuhusu Kesi za Ukwepaji wa Kodi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akihutubia wakati  wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akihutubia wakati
wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017

Mahakama Zamkera JPM, ni Kuhusu Kesi za Ukwepaji wa Kodi

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameelezea kusikitishwa kwake na namna Mahakama inavyoshughulikia kesi zinazohusiana na ukwepaji wa kodi na ametoa wito kwa mahakama na wadau wake kujipanga kukabiliana na dosari hiyo inayorudisha nyuma juhudi za maendeleo ya nchi. Continue reading “Mahakama Zamkera JPM, ni Kuhusu Kesi za Ukwepaji wa Kodi”

Rais Magufuli Amteuwa Jenerali Venance Mabeyo Mkuu wa Majeshi Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Luteni Jenerali Venance Salvatory Mabeyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Luteni Jenerali Venance Salvatory Mabeyo.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli, leo Tarehe 02 Februari, 2017 amemteua Luteni Jenerali Venance S. Mabeyo kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania. Continue reading “Rais Magufuli Amteuwa Jenerali Venance Mabeyo Mkuu wa Majeshi Tanzania”

Rais Magufuli alaani kuuawa kwa Rubani Roger Gower

Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelaani kitendo cha watu wanaosadikiwa kuwa ni majangili kumuua kwa kumpiga risasi Rubani wa helkopta Roger Gower, raia wa Uingereza na kisha kuidondosha helkopta aliyokuwa akiiendesha.

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Jumanne Maghembe akiwa eneo la tukio ilipotunguliwa helkopta ya TANAPA iliyomuua Kept. Roger Gower.

Tukio hilo limetokea wakati alipoungana na Askari wanyamapori waliokuwa wakikabiliana na majangili katika pori la akiba lililopo katika wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu.

Rais Magufuli ameelezea kusikitishwa sana na tukio hilo na ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kuhakikisha waliomuua Rubani Gower na kuidondosha helkopta aliyokuwa akiiendesha wanakamatwa na wanafikishwa mikononi mwa vyombo vya sheria.

Amemtumia salamu za pole, Balozi wa Uingereza hapa nchini kwa kumpoteza raia wake ambaye alikuwa akitoa mchango mkubwa katika kuhifadhi wanyamapori wa hapa nchini Tanzania.

Aidha, Rais Magufuli amesema serikali yake itahakikisha inaendeleza mapambano dhidi ya ujangili kwa nguvu zake zote na kuwataka wananchi na wadau mbalimbali wa hifadhi ya wanyamapori, kutokatishwa tamaa na tukio hili na watoe ushirikiano wa kutosha kuwafichua watu wote wanaojihusisha na ujangili ama biashara ya bidhaa zitokanazo na ujangili.

Katika tukio hilo, pamoja na kumuua Rubani Roger Gower watu hao wanaosadikiwa kuwa majangili wamemjeruhi Askari wanyama pori mmoja na wamewaua tembo watatu.

Continue reading “Rais Magufuli alaani kuuawa kwa Rubani Roger Gower”

Yaliyojiri Leo Ikulu Baada Ya Rais Magufuli Kukutana na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),DPP na Mufti Mkuu wa Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wanne Ikulu Jijini Dar es salaam ambapo pamoja na kutakiana heri ya Mwaka Mpya, wamezungumzia mambo mbalimbali kuhusu mustakabali wa Serikali ya awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

maggg

Akizungumzia yaliyojiri katika Mazungumzo hayo, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Juma Assad amesema wamezungumzia kupunguza gharama za matumizi ya kuendesha serikali na kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
Profesa Assad amebainisha kuwa Rais Magufuli ametaka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ihakikishe Tanzania inaongeza ukusanyaji wa mapato kutoka asilimia 14 ya pato la Taifa (GDP) kwa mujibu wa hesabu zilizofanyika mwaka juzi.
“Hadi Mwaka juzi Tanzania ilikua inakusanya mapato kwa kiwango cha asilimia 14 ya pato la Taifa ikilinganishwa na Kenya ambayo ilikua ikikusanya asilimia 19 ya pato Taifa, na hakuna sababu za Msingi za kwa nini Tanzania iwe nyuma katika ukusanyaji wa mapato hayo” aliongeza Profesa Assad.
Rais Magufuli pia amekutana na Mkurugenzi wa Mashitaka hapa Nchini (DPP) Mheshimiwa Biswalo Eutropius Mganga ambaye amesema mazungumzo yao yalijikita katika suala la kupeana mikakati ya namna ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka inavyopaswa kufanya kazi ili kuendana na kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano isemayo “Hapa Kazi Tu”
Aidha Mganga ameongeza kuwa wamezungumzia umuhimu wa kuwahimiza watanzania kufuata sheria, na kwamba ofisi yake itatekeleza wajibu wake bila kumuonea mtu.
Kiongozi Mwingine aliyekutana na Rais Magufuli ni Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuber Ally ambaye pamoja na kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa juhudi kubwa alizoanza nazo katika uongozi wake, amesema waislamu wote nchini wanamuunga mkono na kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ili aendelee na juhudi hizo.
“Na pia kwa niaba ya Waislamu tunataka kumueleza kwamba kazi anayoifanya ni kazi ambayo tunairidhia na tunamuomba aendelee kuifanya wala asiogope, na kauli yake ya Hapa Kazi Tu iendelee, kwa sababu inaonesha kwamba sasa nchi yetu itakaa mahali pazuri” Alibainisha Mufti Mkuu
Kiongozi Mwingine aliyekutana na Rais Magufuli ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Alhaji Abdallah Majura Bulembo ambaye amempongeza Mheshimiwa Rais kwa kasi nzuri aliyoanza nayo katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015- 2020 na kutaka kasi hiyo iendelee.
Amesema Jumuiya ya Wazazi inaunga mkono kazi kubwa inayofanywa na Rais Magufuli na kwamba Mheshimiwa Rais amemuhakikishia kuwa ataendelea kufanya kazi hizo zaidi katika kutekeleza Ilani ya CCM.
“Tunafurahi kwamba yapo mambo mengi ambayo Rais Magufuli ameanza kuyatekeleza kwa haraka, mojawapo likiwa ni kufutwa kwa ada za shule, na hivi sasa wanafunzi watakwenda shule pasipo kutozwa ada” alisisitiza Alhaji Bulembo
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
04 Januari, 2016