Tag Archives: Liverpool

Rekodi kali kuelekea Man City na Liverpool leo

Kuelekea mchezo wa marudiano leo ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya robo fainali kati ya wenyeji Manchester City dhidi ya Liverpool, hizi ni rekodi ambazo zinaweza kuvunjwa au kuwekwa na timu zote mbili endapo zitapata matokeo chanya.

Continue reading Rekodi kali kuelekea Man City na Liverpool leo

Advertisements

Jurgen Klopp kutua Liverpool Ijumaa!

Klabu ya soka ya Liverpool imetangaza kuwa ina matumaini ya kumteua Jurgen Klopp kuwa meneja mpya wa klabu hiyo ifikapo siku ya ijumaa wiki hii.

 Jurgen-Klopp

Mazungumzo kati ya klabu ya Liverpool na wawakilishi wa Klopp ambaye ni kocha wa zamani wa klabu ya Borussia Dortmund yanaendelea kuangalia uwezekano wa kuchukua nafasi ya meneja aliyetimuliwa Brendan Rodgers. Klopp mwenye miaka 48 raia wa Ujerumani ameweka wazi mipango ya kujiunga na klabu yoyote kwa sasa. Wamiliki wa klabu hiyo wamepanga kupata mwalimu mpya kabla ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tottenham tar 17 mwezi Oktoba.

Katika taarifa iliyotolewa na chama cha mameneja wa ligi hiyo kwa niaba ya Rodgers imeelezea kusikitishwa kwake na tukio la kutimuliwa kwa kocha huyo. ”imekuwa heshima na upendeleo wa kipekee kwangu kuiongoza klabu ya Liverpool hususan katika michezo migumu”alisema Rodgers aliyetimuliwa baada ya suluhu ya bao 1-1 dhidi ya Everton siku ya jumapili.

Brendan Rodgers afukuzwa Liverpool

Klabu ya soka ya Liverpool ya nchini Uingereza imemfukuza Meneja wake Brendan Rodgers baada ya matokeo mabaya ya muda mrefu.

 141216130724_brendan_rodgers_640x360_afp_nocredit

Uamuzi wa kumfuta kazi Rodgers ulifanywa hata kabla ya mchezo ulioisha kwa suluhu dhidi ya Everton ambao uliwaacha Liverpool katika nafasi ya kumi katika msimamo wa ligi ya England.

”Licha ya kuwa huu umekuwa ni uamuzi mgumu,tunaamini itatupa nguvu zaidi uwanjani,”ilisema taarifa ya klabu.

Meneja wa zamani wa klabu ya Chelsea na Real Madrid Carlo Ancelotti,kocha wa Ajax Frank de Boer na meneja wa zamani wa klabu ya Borussia Dortmund wamehusishwa kujiunga na klabu ya Liverpool katika siku za karibuni baada ya timu hiyo kuuanza msimu kwa kusua sua.

STERLING: LIVERPOOL NA MAN CITY ZAKUBALIANA

Klabu ya Manchester City ya Uingereza imekubaliana na wapinzani wao Liverpool dau la pauni milioni £49 kumsajili mshambulizi Raheem Sterling.

Sterling
Sterling

Uhamisho wa mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 20 sasa unategemea makubaliano baina yao na vipimo vya afya.

Sterling alikuwa ameomba kundoka Anfield kabla ya klabu hiyo kukataa dau mbili za Man City mwezi Juni.

Mshambulizi huyo atakuwa mchezaji aliyegharimu pesa nyingi zaidi raia wa Uingereza baada yake kukatalia mbali mshahara wa pauni laki moja kwa juma kutoka Liverpool.

Sterling aliyejiunga na Liverpool akiwa na umri wa miaka 15 kutoka QPR mwezi februari mwaka wa 2010 yuko katika kandarasi inayokamilika mwaka wa 2017.

QPR inatarajiwa kupokea asilimia 20% ya ada ya kukuza kipaji chake kutoka kwa pesa hizo.

Jumamosi iliyopita ,Sterling alikuwa ametajwa katika kikosi kitakachozuru Thailand, Australia na Malaysia, lakini jina lake likaondolewa.

Wachezaji kadha wakongwe wa klabu hiyo wamemkashifu kwa kutaka kuihama klabu hiyo tangu kocha Brendan Rodgers na mkurugenzi mkuu Ian Ayre kutangaza kuwa alikuwa na nia ya kuihama.

Hivi majuzi utafiti ulimorodhesha kama mchezaji mwenye thamani zaidi barani ulaya.

Mchezaji wa Paris St-Germain Marquinhos alikuwa wapili huku Memphis Depay aliyeihamia Manchester United akiorodheshwa tatu bora.

BALOTELLI HAJAREJEA KAMBINI- LIVERPOOL

Mshambulizi wa Liverpool na Italia , Mario Balotelli hajarejea kambini Anfield kwa mazoezi ya kabla ya kuanza kwa msimu mpya.

Mario Balotelli
Mario Balotelli

Muitaliano huyo ambaye hakuwa na msimu wa kufana alipojiunga na the Reds anasemekana kuwa alifiwa.

The Reds’ walirejea katika kambi ya mazoezi siku ya jumatatu baada ya likizo ndefu ya msimu wa jua.

 “ningependa kuwashukuru mashabiki wangu wote”

”Familia yangu inawashukuru pia”alisema mshambulizi huyo machachari.

Balotelli mwenye umri wa miaka 24 anatarajiwa kujiunga na kikosi hicho cha Liverpool kabla ya ziara ya kujipima nguvu mashariki ya mbali na Australia.

Mario Balotelli
Mario Balotelli

Tangu ajiunge na the Reds mshambulizi huyo wa zamani wa Manchester City hakunga’ara kama ilivyotarajiwa baada ya kununuliwa kwa kima cha pauni milioni £16m mwezi Agosti.

Alifunga mabao 4 ikiwemo moja pekee katika ligi ya premia na hakuweza kuhakikishiwa nafasi ya timu ya kwanza licha ya kutokuwepo kwa nyota kutoka Uruguay Luis Suarez.

LIVERPOOL YAMSAJILI FIRMINO WA BRAZIL

Klabu ya Liverpool imemsajili mshambuliaji wa Brazil Roberto Firmino kutoka klabu ya Hoffenheim kwa kanadarasi ya miaka mitano itakayogharimu pauni millioni 29.

 Mkataba huo utaandamana na ukaguzi wa kimatibabu ambao utafanyika baada ya mchezaji huyo kurudi kutoka Chile ambapo amekuwa akiichezea Brazil katika michuano ya Copa America.

Firmino ambaye amefunga mabao 47 katika mechi 151 akiwa katika kilabu ya Hoffenheim atakuwa mchezaji wa pili wa Liverpool aliyeghali mno.

 Kilabu hiyo ya Anfield ilimfanya mchezaji Andy Carroll kuwa mchezaji ghali alipojiunga nayo kwa kitita cha pauni milioni 35 kutoka Newcastle mwaka 2011

LIVERPOOL YAKATAA KUMUUZA STERLING

Klabu ya Liverpool imekataa rasmi ombi la pili la Manchester City la kutaka kumsajili mshambuliaji wa Uingereza Raheem Sterling.

 150618172755_raheem_sterling_640x360_reuters_nocredit

Inaaminika kuwa ombi hilo jipya lilikuwa la kitita cha pauni milioni 35.5 ambacho kingeongezwa na kufika pauni milioni 40.

Sterling mwenye umri wa miaka 20 ambaye amehusishwa na Arsenal pamoja na Real Madrid ana thamani ya pauni milioni 50 kulingana na Liverpool.

Wiki iliopita Liverpool ilikataa kitita cha pauni milioni 25 kutoka kwa Manchester City.

Sterling alijiunga na Liverpool kutoka QPR mwaka 2010 na sasa yuko katika kandarasi hadi mwaka 2017,lakini amekataa ombi la malipo ya kitita cha pauni 100,000 kwa wiki.