Tag Archives: Paul Makonda

Wanaume 18 Wakubali Kupimwa DNA kwa Makonda

WANAUME 18 kati ya waliofika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kuhojiwa kuhusu kutelekeza watoto wamekubali kupimwa vinasaba (DNA) na Mkemia Mkuu wa Serikali, taarifa iliyotolewa jana na Paul Makonda ilisema. Continue reading Wanaume 18 Wakubali Kupimwa DNA kwa Makonda

Advertisements

Paul Makonda Akanusha Kuwaita Edward Lowasa, Mbowe

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni zikiwa na orodha ya majina ya watu akiwemo Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowasa na baadhi ya wabunge kuwa wameitwa ofisini kwake kwa madai ya kutekeleza watoto wao. Continue reading Paul Makonda Akanusha Kuwaita Edward Lowasa, Mbowe

“Tutakutangaza hadharani mkeo ajue” – Paul Makonda

Paul Makonda amefunguka na kusema wanaume ambao wamewazalisha wanawake na kuwatelekeza bila kuwapa matunzo pindi watakapoitwa wakikaidi wito huo kwa lengo la kulinda ndoa zao basi watawatangaza hadharani ili wake zao wajue wana watoto nje ya ndoa.

Continue reading “Tutakutangaza hadharani mkeo ajue” – Paul Makonda

MAKONDA ATOA MISAADA KWA WAJAWAZITO WATAKAOJIFUNGUA PASAKA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda leo ametoa zawadi ya vifaa tiba vya Mama mzazi kwaajili ya kujifungulia (Delivery Packs) 200 vyenye thamani ya zaidi ya shilingi million 20 Kama zawadi yake ya sikukuu ya pasaka kwa kinamama watakaojifungua kwenye msimu huu wa pasaka. Continue reading MAKONDA ATOA MISAADA KWA WAJAWAZITO WATAKAOJIFUNGUA PASAKA

MAKONDA AFANIKISHA SAFARI NA MATIBABU YA AHMED ALBAITY CHINA

NDOTO na shauku ya kijana Ahmed Albaity alieteseka kwa zaidi ya Miaka 10 Kitandani kwa kushindwa kumudu gharama za matibabu leo imebadilika kuwa furaha baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda kumkabidhi Tiketi za Ndege za watu Wanne kwaajili ya safari ya kwenda kupatiwa matibabu Nchini China kwenye Hospital ya Beijing Puhua International huku akijitolea pia kugharamia fedha za Matibabu na Malazi.

 

RC Makonda alitoa ahadi kumsaidia Ahmed Albaity wakati wa Zoezi la Upimaji Afya Bure kwenye Meli ya Jeshi la China mwishoni mwa Mwaka Jana baada ya kugundulika Ahmed anahitaji Matibabu Maalum ambayo hayapatikani kokote kule duniani isipokuwa China, jambo lililomfanya RC Makonda kutokwa na Machozi na Kuhaidi Kumpeleka kwenye matibabu kwa gharama yoyote ile Maumivu na Mateso anayopitia kijana huyo.

 

Ahmed Albaity anasumbuliwa na tatizo la uti wa mgongo baada ya kuanguka na kuvunjika Shingo alipokuwa akiogelea ambapo kwa sindano moja pekee inagharimu Dollars 26,000/= sawa na shillingi million 52.

 

RC Makonda amesema Ahmed atasafiri Nchini China Siku ya Jumapili akiongozana na watu watatu wa kumsaidia kumuhudumia ambapo gharama zake ni zaidi ya Shilingi Million 100.

 

Aidha RC Makonda amesema Shauku yake ni kugusa maisha ya Mwananchi hata kama ni mmoja atakaekwenda mbele za Mungu na kusema Asante Mungu kwa kutupatia viongozi wetu, ifike mahali tumtumikie Mungu katika nafasi zetu, na katika hilo watu wote watakuwa Sawa na tutawahudumia bila kutarajia chochote kutoka kwao kama sehemu ya utumishi wetu ambapo amewashukuru watu wote waliomchangia na kufanikisha matibabu.

 

 

Hata hivyo RC Makonda ametoa wito kwa wananchi wa dini zote kumuombea Ahmed ili aweze kupona na kuendelea na shughuli za ujenzi wa Taifa.

 

Kwa upande wa Ahmed Albaity amemshukuru RC Makonda kwa moyo wa ukarimu aliouonyesha ambapo ameeleza kuwa ameishi kwa mateso muda mrefu kutokana na kukosa uwezo wa kumudu gharama za matibabu.

 Aidha amesema alipokuwa akiomba watu wamchangie wapo waliokuwa wakimvunja moyo kwa kumwambia hawezi kupona lakini RC Makonda ameonyesha moyo wa kipekee.

Continue reading MAKONDA AFANIKISHA SAFARI NA MATIBABU YA AHMED ALBAITY CHINA